Waebrania 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 3 (Swahili) Hebrews 3 (English)

Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, Waebrania 3:1

Therefore, holy brothers, partakers of a heavenly calling, consider the Apostle and High Priest of our confession, Jesus;

aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. Waebrania 3:2

who was faithful to him who appointed him, as also was Moses in all his house.

Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. Waebrania 3:3

For he has been counted worthy of more glory than Moses, inasmuch as he who built the house has more honor than the house.

Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. Waebrania 3:4

For every house is built by someone; but he who built all things is God.

Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; Waebrania 3:5

Moses indeed was faithful in all his house as a servant, for a testimony of those things which were afterward to be spoken,

bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho. Waebrania 3:6

but Christ is faithful as a Son over his house; whose house we are, if we hold fast our confidence and the glorying of our hope firm to the end.

Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Waebrania 3:7

Therefore, even as the Holy Spirit says, "Today if you will hear his voice,

Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa, Waebrania 3:8

Don't harden your hearts, as in the provocation, Like as in the day of the trial in the wilderness,

Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini. Waebrania 3:9

Where your fathers tested me by proving me, And saw my works for forty years.

Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu; Waebrania 3:10

Therefore I was displeased with that generation, And said, 'They always err in their heart, But they didn't know my ways;'

Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu. Waebrania 3:11

As I swore in my wrath, 'They will not enter into my rest.'"

Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Waebrania 3:12

Beware, brothers, lest perhaps there be in any one of you an evil heart of unbelief, in falling away from the living God;

Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Waebrania 3:13

but exhort one another day by day, so long as it is called "today;" lest any one of you be hardened by the deceitfulness of sin.

Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; Waebrania 3:14

For we have become partakers of Christ, if we hold fast the beginning of our confidence firm to the end:

hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. Waebrania 3:15

while it is said, "Today if you will hear his voice, Don't harden your hearts, as in the rebellion."

Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? Waebrania 3:16

For who, when they heard, rebelled? No, didn't all those who came out of Egypt by Moses?

Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Waebrania 3:17

With whom was he displeased forty years? Wasn't it with those who sinned, whose bodies fell in the wilderness?

Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Waebrania 3:18

To whom did he swear that they wouldn't enter into his rest, but to those who were disobedient?

Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Waebrania 3:19

We see that they were not able to enter in because of unbelief.