Waebrania 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 4 (Swahili) Hebrews 4 (English)

Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Waebrania 4:1

Let us fear therefore, lest perhaps a promise being left of entering into his rest, anyone of you should seem to have come short of it.

Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Waebrania 4:2

For indeed we have had good news preached to us, even as they also did, but the word they heard didn't profit them, because it wasn't mixed with faith by those who heard.

Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: Waebrania 4:3

For we who have believed do enter into that rest, even as he has said, "As I swore in my wrath, they will not enter into my rest;" although the works were finished from the foundation of the world.

Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; Waebrania 4:4

For he has said this somewhere about the seventh day, "God rested on the seventh day from all his works;"

na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. Waebrania 4:5

and in this place again, "They will not enter into my rest."

Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, Waebrania 4:6

Seeing therefore it remains that some should enter therein, and they to whom the good news was before preached failed to enter in because of disobedience,

aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. Waebrania 4:7

he again defines a certain day, today, saying through David so long a time afterward (just as has been said), "Today if you will hear his voice, Don't harden your hearts."

Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. Waebrania 4:8

For if Joshua had given them rest, he would not have spoken afterward of another day.

Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Waebrania 4:9

There remains therefore a Sabbath rest for the people of God.

Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Waebrania 4:10

For he who has entered into his rest has himself also rested from his works, as God did from his.

Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. Waebrania 4:11

Let us therefore give diligence to enter into that rest, lest anyone fall after the same example of disobedience.

Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Waebrania 4:12

For the word of God is living, and active, and sharper than any two-edged sword, and piercing even to the dividing of soul and spirit, of both joints and marrow, and is able to discern the thoughts and intentions of the heart.

Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. Waebrania 4:13

There is no creature that is hidden from his sight, but all things are naked and laid open before the eyes of him with whom we have to do.

Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Waebrania 4:14

Having then a great high priest, who has passed through the heavens, Jesus, the Son of God, let us hold tightly to our confession.

Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Waebrania 4:15

For we don't have a high priest who can't be touched with the feeling of our infirmities, but one who has been in all points tempted like we are, yet without sin.

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. Waebrania 4:16

Let us therefore draw near with boldness to the throne of grace, that we may receive mercy, and may find grace for help in time of need.