Sifa Lyrics

Nichukue by Semeiyan cover art

Semeiyan - Nichukue Lyrics

Artist:
Semeiyan

Lyrics

Nichukue, nitengeneze
Niwe chombo chako Bwana
Nichukue, nifinyange
Niwe chombo cha heshima

Hili ni ombi baba naomba, nimekosa Baba eeh,
Makosa yangu hayahesabiki, sistahili Baba mbele zako,
Na sasa Baba naja

Kama vile Daudi aliomba, maombi yake Ukayasikia,
Kama vile Paulo na Silah, waliomba Baba eeh
Nakuomba Baba nisikie
Kama vile Daudi aliomba, maombi yake Ukayasikia,
Kama vile Paulo na Silah, waliomba Baba eeh
Nakuomba Baba nisikie

Nichukue, nitengeneze
Niwe chombo chako Bwana
Nichukue, nifinyange
Niwe chombo cha heshima

Moyo wangu wakutamani, njia zako kuzifuata
Nitakase nikupendeze, Wewe ndiwe uhai wangu
Damu yako Baba yanitosha

Video