Tufani inapovuma,
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha,
Mkononi mwa Mungu,
Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Pengine kuna taabu,
Yanisongeza kwake,
Najua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.
Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Adui wakiniudhi,
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza,
Vyote viwe baraka.
Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Niishipo duniani,
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni,
Nitakaa salama.
Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.
Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?
Psalms 27 : 5Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
Psalms 55 : 12Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.