MTETEZI WANGU YU HAI Lyrics - Angela K Wambua Music

Angela K Wambua Music John Kay swahili

MTETEZI WANGU YU HAI Lyrics

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

Naipotelea mbali siku ya kuzaliwa kwangu,iwe kisa tupu mwanga usiangazie nikaweka tumaini kwa mwanadamu nikabaki pweke 
niliokula nao meza moja kaniinulia visigino,ole wangu kuweka tumaini kwa wanadamu,kazi sina,chakula,mavazi sina,magonjwa yaniandama mungu wangu,mungu wangu huwezi muache mwenye haki anguke.

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

Babaa,Babaa
machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku
wengi wananiambia mchana kutwa yupo wapi Mungu wakoo
Babaa,Babaa
ikiwezekana Kikombe hiki kiniebuke
lakini si kama nitakavyo mimi bali utakavyo Baba

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

Na wamama aweza sahau mtoto anayemnyonyesha, wasema mimi wako huwezi nisahau na mapito ni kipimo cha imani yangu ni ya muda tu,uniandalie meza kubwa mbele ya watezi,Nile,Ninywe wakiona Mungu tuma neno moja hali yangu ibadilike,tuma neno moja waibike wajue hauchelewi wakati wako ndio bora.

Ninajua Baba ndiye mtetezi wangu
Najua mtetezi wangu yu hai hawezi niacha,na baada ya mapito nitamuona kwa macho yangu na si ya mwengine

MTETEZI WANGU YU HAI Video