Ezra 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezra 9 (Swahili) Ezra 9 (English)

Na mambo hayo yalipokwisha kutendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, wamefanya sawasawa na machukizo yao, yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori. Ezra 9:1

Now when these things were done, the princes drew near to me, saying, The people of Israel, and the priests and the Levites, have not separated themselves from the peoples of the lands, [doing] according to their abominations, even of the Canaanites, the Hittites, the Perizzites, the Jebusites, the Ammonites, the Moabites, the Egyptians, and the Amorites.

Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili. Ezra 9:2

For they have taken of their daughters for themselves and for their sons, so that the holy seed have mixed themselves with the peoples of the lands: yes, the hand of the princes and rulers has been chief in this trespass.

Nami niliposikia hayo, nikararua nguo yangu na joho yangu, nikang'oa nywele za kichwa changu, na ndevu zangu, nikaketi kwa mshangao. Ezra 9:3

When I heard this thing, I tore my garment and my robe, and plucked off the hair of my head and of my beard, and sat down confounded.

Ndipo wakanikusanyikia watu wote walioyatetemekea maneno ya Mungu wa Israeli, kwa sababu ya lile kosa la watu wa uhamisho; nami nikaketi kwa mshangao hata wakati wa sadaka ya jioni. Ezra 9:4

Then were assembled to me everyone who trembled at the words of the God of Israel, because of the trespass of them of the captivity; and I sat confounded until the evening offering.

Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu; Ezra 9:5

At the evening offering I arose up from my humiliation, even with my garment and my robe torn; and I fell on my knees, and spread out my hands to Yahweh my God;

nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni. Ezra 9:6

and I said, my God, I am ashamed and blush to lift up my face to you, my God; for our iniquities are increased over our head, and our guiltiness is grown up to the heavens.

Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo. Ezra 9:7

Since the days of our fathers we have been exceeding guilty to this day; and for our iniquities have we, our kings, and our priests, been delivered into the hand of the kings of the lands, to the sword, to captivity, and to plunder, and to confusion of face, as it is this day.

Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu. Ezra 9:8

Now for a little moment grace has been shown from Yahweh our God, to leave us a remnant to escape, and to give us a nail in his holy place, that our God may lighten our eyes, and give us a little reviving in our bondage.

Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, kuisimamisha nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu. Ezra 9:9

For we are bondservants; yet our God has not forsaken us in our bondage, but has extended loving kindness to us in the sight of the kings of Persia, to give us a reviving, to set up the house of our God, and to repair the ruins of it, and to give us a wall in Judah and in Jerusalem.

Na sasa, Ee Mungu wetu, tuseme nini baada ya hayo? Maana tumeziacha amri zako, Ezra 9:10

Now, our God, what shall we say after this? for we have forsaken your commandments,

ulizoziamuru kwa midomo ya watumishi wako, manabii, ukisema, Nchi ile, mnayoiendea ili kuimiliki, ni nchi ya uchafu, kwa sababu ya uchafu wa watu wa nchi zile, kwa ajili ya machukizo yao, yaliyoijaza tangu upande huu mpaka upande huu, kwa uchafu wao. Ezra 9:11

which you have commanded by your servants the prophets, saying, The land, to which you go to possess it, is an unclean land through the uncleanness of the peoples of the lands, through their abominations, which have filled it from one end to another with their filthiness:

Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele. Ezra 9:12

now therefore don't give your daughters to their sons, neither take their daughters to your sons, nor seek their peace or their prosperity forever; that you may be strong, and eat the good of the land, and leave it for an inheritance to your children forever.

Na baada ya hayo yote yaliyotupata kwa sababu ya matendo yetu mabaya, na kwa sababu ya hatia yetu iliyo kuu, ikiwa wewe Mungu wetu hukutuadhibu kama tulivyostahili kwa maovu yetu, tena umetupa mabaki; Ezra 9:13

After all that is come on us for our evil deeds, and for our great guilt, seeing that you our God have punished us less than our iniquities deserve, and have given us such a remnant,

je! Tuzivunje tena amri zako, tukajiunge na watu wanaotenda machukizo hayo, kwa kuoana nao? Je! Usingekasirika nasi hata kutuangamiza kabisa, pasisalie mabaki yo yote, wala mtu wa kuokoka? Ezra 9:14

shall we again break your commandments, and join in affinity with the peoples that do these abominations? would not you be angry with us until you had consumed us, so that there should be no remnant, nor any to escape?

Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili. Ezra 9:15

Yahweh, the God of Israel, you are righteous; for we are left a remnant that is escaped, as it is this day: behold, we are before you in our guiltiness; for none can stand before you because of this.