1 Petro 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Petro 3 (Swahili) 1st Peter 3 (English)

Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 1 Petro 3:1

In like manner, wives, be in subjection to your own husbands; so that, even if any don't obey the Word, they may be won by the behavior of their wives without a word;

wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 1 Petro 3:2

seeing your pure behavior in fear.

Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 1 Petro 3:3

Let your beauty be not just the outward adorning of braiding the hair, and of wearing jewels of gold, or of putting on fine clothing;

bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 1 Petro 3:4

but in the hidden person of the heart, in the incorruptible adornment of a gentle and quiet spirit, which is in the sight of God very precious.

Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 1 Petro 3:5

For this is how the holy women before, who hoped in God, also adorned themselves, being in subjection to their own husbands:

Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote. 1 Petro 3:6

as Sarah obeyed Abraham, calling him lord, whose children you now are, if you do well, and are not put in fear by any terror.

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. 1 Petro 3:7

You husbands, in like manner, live with your wives according to knowledge, giving honor to the woman, as to the weaker vessel, as being also joint heirs of the grace of life; that your prayers may not be hindered.

Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; 1 Petro 3:8

Finally, be all like-minded, compassionate, loving as brothers, tenderhearted, courteous,

watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. 1 Petro 3:9

not rendering evil for evil, or reviling for reviling; but instead blessing; knowing that to this were you called, that you may inherit a blessing.

Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. 1 Petro 3:10

For, "He who would love life, And see good days, Let him keep his tongue from evil, And his lips from speaking deceit.

Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. 1 Petro 3:11

Let him turn away from evil, and do good. Let him seek peace, and pursue it.

Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. 1 Petro 3:12

For the eyes of the Lord are on the righteous, And his ears open to their prayer; But the face of the Lord is against those who do evil."

Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? 1 Petro 3:13

Now who is he who will harm you, if you become imitators of that which is good?

Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. 1 Petro 3:14

But even if you should suffer for righteousness' sake, you are blessed. "Don't fear what they fear, neither be troubled."

Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 1 Petro 3:15

But sanctify the Lord God in your hearts; and always be ready to give an answer to everyone who asks you a reason concerning the hope that is in you, with humility and fear:

Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. 1 Petro 3:16

having a good conscience; that, while you are spoken against as evildoers, they may be disappointed who curse your good manner of life in Christ.

Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 1 Petro 3:17

For it is better, if the will of God should so will, that you suffer for doing well than for doing evil.

Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 1 Petro 3:18

Because Christ also suffered for sins once, the righteous for the unrighteous, that he might bring you to God; being put to death in the flesh, but made alive in the spirit;

ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 1 Petro 3:19

in which he also went and preached to the spirits in prison,

watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 1 Petro 3:20

who before were disobedient, when God waited patiently in the days of Noah, while the ark was being built. In it, few, that is, eight souls, were saved through water.

Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 1 Petro 3:21

This is a symbol of baptism, which now saves you-- not the putting away of the filth of the flesh, but the answer of a good conscience toward God, through the resurrection of Jesus Christ,

Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake. 1 Petro 3:22

who is at the right hand of God, having gone into heaven, angels and authorities and powers being made subject to him.