1 Petro 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Petro 1 (Swahili) 1st Peter 1 (English)

Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia; 1 Petro 1:1

Peter, an apostle of Jesus Christ, to the chosen ones who are living as strangers in the Dispersion in Pontus, Galatia, Cappadocia, Asia, and Bithynia,

kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu. 1 Petro 1:2

according to the foreknowledge of God the Father, in sanctification of the Spirit, that you may obey Jesus Christ and be sprinkled in his blood: Grace to you and peace be multiplied.

Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 1 Petro 1:3

Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ, who according to his great mercy became our father again to a living hope through the resurrection of Jesus Christ from the dead,

tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 1 Petro 1:4

to an incorruptible and undefiled inheritance that doesn't fade away, reserved in heaven for you,

Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 1 Petro 1:5

who by the power of God are guarded through faith for a salvation ready to be revealed in the last time.

Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 1 Petro 1:6

Wherein you greatly rejoice, though now for a little while, if need be, you have been put to grief in various trials,

ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 1 Petro 1:7

that the proof of your faith, which is more precious than gold that perishes even though it is tested by fire, may be found to result in praise, glory, and honor at the revelation of Jesus Christ--

Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, 1 Petro 1:8

whom not having known you love; in whom, though now you don't see him, yet believing, you rejoice greatly with joy unspeakable and full of glory--

katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 1 Petro 1:9

receiving the result of your faith, the salvation of your souls.

Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 1 Petro 1:10

Concerning this salvation, the prophets sought and searched diligently, who prophesied of the grace that would come to you,

Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 1 Petro 1:11

searching for who or what kind of time the Spirit of Christ, which was in them, pointed to, when he predicted the sufferings of Christ, and the glories that would follow them.

Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. 1 Petro 1:12

To them it was revealed, that not to themselves, but to you, did they minister these things, which now have been announced to you through those who preached the Gospel to you by the Holy Spirit sent out from heaven; which things angels desire to look into.

Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 1 Petro 1:13

Therefore, prepare your minds for action,{Literally, "gird up the loins of your mind"} be sober and set your hope fully on the grace that will be brought to you at the revelation of Jesus Christ--

Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 1 Petro 1:14

as children of obedience, not conforming yourselves according to your former lusts as in your ignorance,

bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 1 Petro 1:15

but just as he who called you is holy, you yourselves also be holy in all of your behavior;

kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 1 Petro 1:16

because it is written, "You shall be holy; for I am holy."

Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 1 Petro 1:17

If you call on him as Father, who without respect of persons judges according to each man's work, pass the time of your living as strangers here in reverent fear:

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 1 Petro 1:18

knowing that you were redeemed, not with corruptible things, with silver or gold, from the useless way of life handed down from your fathers,

bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 1 Petro 1:19

but with precious blood, as of a lamb without spot, the blood of Christ;

Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 1 Petro 1:20

who was foreknown indeed before the foundation of the world, but was revealed at the end of times for your sake,

ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. 1 Petro 1:21

who through him are believers in God, who raised him from the dead, and gave him glory; so that your faith and hope might be in God.

Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. 1 Petro 1:22

Seeing you have purified your souls in your obedience to the truth through the Spirit in sincere brotherly affection, love one another from the heart fervently:

Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 1 Petro 1:23

having been born again, not of corruptible seed, but of incorruptible, through the word of God, which lives and remains forever.

Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; 1 Petro 1:24

For, "All flesh is like grass, And all of man's glory like the flower in the grass. The grass withers, and its flower falls;

Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu. 1 Petro 1:25

But the Lord's word endures forever." This is the word of good news which was preached to you.