1 Wakorintho BSB

1 Wakorintho 3

1st Corinthians Chapter 3

1
Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.
Brothers, I could not address you as spiritual, but as worldly—as infants in Christ.
2
Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,
I gave you milk, not solid food, for you were not yet ready for solid food. In fact, you are still not ready,
3
kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?
for you are still worldly. For since there is jealousy and dissension among you, are you not worldly? Are you not walking in the way of man?
4
Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
For when one of you says, “I follow Paul,” and another, “I follow Apollos,” are you not mere men?
5
Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
What then is Apollos? And what is Paul? They are servants through whom you believed, as the Lord has assigned to each his role.
6
Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
I planted the seed and Apollos watered it, but God made it grow.
7
Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
So neither he who plants nor he who waters is anything, but only God, who makes things grow.
8
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.
He who plants and he who waters are one in purpose, and each will be rewarded according to his own labor.
9
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
For we are God’s fellow workers; you are God’s field, God’s building.
10
Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
By the grace God has given me, I laid a foundation as an expert builder, and someone else is building on it. But each one must be careful how he builds.
11
Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
For no one can lay a foundation other than the one already laid, which is Jesus Christ.
12
Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.
If anyone builds on this foundation using gold, silver, precious stones, wood, hay, or straw,
13
Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
his workmanship will be evident, because the Day will bring it to light. It will be revealed with fire, and the fire will prove the quality of each man’s work.
14
Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
If what he has built survives, he will receive a reward.
15
Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
If it is burned up, he will suffer loss. He himself will be saved, but only as if through the flames.
16
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Do you not know that you yourselves are God’s temple, and that God’s Spirit dwells in you?
17
Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
If anyone destroys God’s temple, God will destroy him; for God’s temple is holy, and you are that temple.
18
Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
Let no one deceive himself. If any of you thinks he is wise in this age, he should become a fool, so that he may become wise.
19
Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.
For the wisdom of this world is foolishness in God’s sight. As it is written: “He catches the wise in their craftiness.”
20
Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.
And again, “The Lord knows that the thoughts of the wise are futile.”
21
Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;
Therefore, stop boasting in men. All things are yours,
22
kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu;
whether Paul or Apollos or Cephas or the world or life or death or the present or the future. All of them belong to you,
23
nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
and you belong to Christ, and Christ belongs to God.

Chagua Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16