1 Wakorintho 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 2 (Swahili) 1st Corinthians 2 (English)

Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. 1 Wakorintho 2:1

When I came to you, brothers, I didn't come with excellence of speech or of wisdom, proclaiming to you the testimony of God.

Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. 1 Wakorintho 2:2

For I determined not to know anything among you, except Jesus Christ, and him crucified.

Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. 1 Wakorintho 2:3

I was with you in weakness, in fear, and in much trembling.

Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, 1 Wakorintho 2:4

My speech and my preaching were not in persuasive words of human wisdom, but in demonstration of the Spirit and of power,

ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. 1 Wakorintho 2:5

that your faith wouldn't stand in the wisdom of men, but in the power of God.

Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; 1 Wakorintho 2:6

We speak wisdom, however, among those who are full grown; yet a wisdom not of this world, nor of the rulers of this world, who are coming to nothing.

bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 1 Wakorintho 2:7

But we speak God's wisdom in a mystery, the wisdom that has been hidden, which God foreordained before the worlds for our glory,

ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; 1 Wakorintho 2:8

which none of the rulers of this world has known. For had they known it, they wouldn't have crucified the Lord of glory.

lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 1 Wakorintho 2:9

But as it is written, "Things which an eye didn't see, and an ear didn't hear, Which didn't enter into the heart of man, These God has prepared for those who love him."

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 1 Wakorintho 2:10

But to us, God revealed them through the Spirit. For the Spirit searches all things, yes, the deep things of God.

Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 1 Wakorintho 2:11

For who among men knows the things of a man, except the spirit of the man, which is in him? Even so, no one knows the things of God, except God's Spirit.

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 1 Wakorintho 2:12

But we received, not the spirit of the world, but the Spirit which is from God, that we might know the things that were freely given to us by God.

Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 1 Wakorintho 2:13

Which things also we speak, not in words which man's wisdom teaches, but which the Holy Spirit teaches, comparing spiritual things with spiritual things.

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 1 Wakorintho 2:14

Now the natural man doesn't receive the things of God's Spirit, for they are foolishness to him, and he can't know them, because they are spiritually discerned.

Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 1 Wakorintho 2:15

But he who is spiritual discerns all things, and he himself is judged by no one.

Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. 1 Wakorintho 2:16

"For who has known the mind of the Lord, that he should instruct him?" But we have Christ's mind.