1 Wakorintho 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 1 (Swahili) 1st Corinthians 1 (English)

Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 1 Wakorintho 1:1

Paul, called to be an apostle of Jesus Christ through the will of God, and our brother Sosthenes,

kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. 1 Wakorintho 1:2

to the assembly of God which is at Corinth; those who are sanctified in Christ Jesus, called to be saints, with all who call on the name of our Lord Jesus Christ in every place, both theirs and ours:

Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 1 Wakorintho 1:3

Grace to you and peace from God our Father and the Lord Jesus Christ.

Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; 1 Wakorintho 1:4

I always thank my God concerning you, for the grace of God which was given you in Christ Jesus;

kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; 1 Wakorintho 1:5

that in everything you were enriched in him, in all speech and all knowledge;

kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu; 1 Wakorintho 1:6

even as the testimony of Christ was confirmed in you:

hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 1 Wakorintho 1:7

so that you come behind in no gift; waiting for the revelation of our Lord Jesus Christ;

ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 1 Wakorintho 1:8

who will also confirm you until the end, blameless in the day of our Lord Jesus Christ.

Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu. 1 Wakorintho 1:9

God is faithful, through whom you were called into the fellowship of his Son, Jesus Christ, our Lord.

Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 1 Wakorintho 1:10

Now I beg you, brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} through the name of our Lord, Jesus Christ, that you all speak the same thing and that there be no divisions among you, but that you be perfected together in the same mind and in the same judgment.

Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. 1 Wakorintho 1:11

For it has been reported to me concerning you, my brothers, by those who are from Chloe's household, that there are contentions among you.

Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. 1 Wakorintho 1:12

Now I mean this, that each one of you says, "I follow Paul," "I follow Apollos," "I follow Cephas," and, "I follow Christ."

Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? 1 Wakorintho 1:13

Is Christ divided? Was Paul crucified for you? Or were you baptized into the name of Paul?

Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; 1 Wakorintho 1:14

I thank God that I baptized none of you, except Crispus and Gaius,

mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 1 Wakorintho 1:15

so that no one should say that I had baptized you into my own name.

Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine. 1 Wakorintho 1:16

(I also baptized the household of Stephanas; besides them, I don't know whether I baptized any other.)

Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika. 1 Wakorintho 1:17

For Christ sent me not to baptize, but to preach the Gospel--not in wisdom of words, so that the cross of Christ wouldn't be made void.

Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 1 Wakorintho 1:18

For the word of the cross is foolishness to those who are dying, but to us who are saved it is the power of God.

Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. 1 Wakorintho 1:19

For it is written, "I will destroy the wisdom of the wise, I will bring the discernment of the discerning to nothing."

Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 1 Wakorintho 1:20

Where is the wise? Where is the scribe? Where is the lawyer of this world? Hasn't God made foolish the wisdom of this world?

Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. 1 Wakorintho 1:21

For seeing that in the wisdom of God, the world through its wisdom didn't know God, it was God's good pleasure through the foolishness of the preaching to save those who believe.

Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; 1 Wakorintho 1:22

For Jews ask for signs, Greeks seek after wisdom,

bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 1 Wakorintho 1:23

but we preach Christ crucified; a stumbling block to Jews, and foolishness to Greeks,

bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 1 Wakorintho 1:24

but to those who are called, both Jews and Greeks, Christ is the power of God and the wisdom of God.

Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. 1 Wakorintho 1:25

Because the foolishness of God is wiser than men, and the weakness of God is stronger than men.

Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 1 Wakorintho 1:26

For you see your calling, brothers, that not many are wise according to the flesh, not many mighty, and not many noble;

bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 1 Wakorintho 1:27

but God chose the foolish things of the world that he might put to shame those who are wise. God chose the weak things of the world, that he might put to shame the things that are strong;

tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 1 Wakorintho 1:28

and God chose the lowly things of the world, and the things that are despised, and the things that are not, that he might bring to nothing the things that are:

mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 1 Wakorintho 1:29

that no flesh should boast before God.

Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 1 Wakorintho 1:30

But of him, you are in Christ Jesus, who was made to us wisdom from God, and righteousness and sanctification, and redemption:

kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana. 1 Wakorintho 1:31

that, according as it is written, "He who boasts, let him boast in the Lord."