Ruthu 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ruthu 2 (Swahili) Ruth 2 (English)

Basi huyo Naomi alikuwa na ndugu ya mumewe, mtu mkuu mwenye mali, wa jamaa yake Elimeleki, na jina lake aliitwa Boazi. Ruthu 2:1

Naomi had a kinsman of her husband's, a mighty man of wealth, of the family of Elimelech, and his name was Boaz.

Naye Ruthuu Mmoabi akamwambia Naomi, Sasa niende kondeni, niokote masazo ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. Ruthu 2:2

Ruth the Moabitess said to Naomi, Let me now go to the field, and glean among the ears of grain after him in whose sight I shall find favor. She said to her, Go, my daughter.

Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki. Ruthu 2:3

She went, and came and gleaned in the field after the reapers: and she happened to come to the portion of the field belonging to Boaz, who was of the family of Elimelech.

Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu kawaamkia wavunaji, akasema, Bwana akae nanyi. Nao wakamwitikia, Bwana na akubariki. Ruthu 2:4

Behold, Boaz came from Bethlehem, and said to the reapers, Yahweh be with you. They answered him, Yahweh bless you.

Kisha Boazi akamwuliza mtumishi aliyewasimamia wavunaji, Na huyu je! Ni msichana wa nani? Ruthu 2:5

Then said Boaz to his servant who was set over the reapers, Whose young lady is this?

Yule msimamizi aliyewasimamia wavunaji akajibu, akasema, Ni yule msichana Mmoabi aliyerudi pamoja na Naomi, kutoka nchi ya Moabu; Ruthu 2:6

The servant who was set over the reapers answered, It is the Moabite lady who came back with Naomi out of the country of Moab:

naye akasema, Tafadhali niruhusu kuokota masazo, na kukusanya nyuma ya wavunaji kati ya miganda; basi akaja, naye ameshinda tangu asubuhi hata sasa, isipokuwa alikaa nyumbani kitambo kidogo. Ruthu 2:7

She said, Please let me glean and gather after the reapers among the sheaves. So she came, and has continued even from the morning until now, except that she stayed a little in the house.

Basi Boazi akamwambia Ruthuu, Mwanangu, sikiliza; wewe usiende kuokota masazo katika shamba lingine, wala usiondoke hapa, lakini ukae papa hapa karibu na wasichana wangu. Ruthu 2:8

Then said Boaz to Ruth, Don't you hear, my daughter? Don't go to glean in another field, neither pass from hence, but abide here fast by my maidens.

Macho yako na yaelekee konde walivunalo, ufuatane nao; je! Sikuwaagiza vijana wasikuguse? Tena, ukiona kiu, uende kwenye vyombo, nawe uyanywe waliyoyateka hao vijana. Ruthu 2:9

Let your eyes be on the field that they reap, and go after them: haven't I charged the young men that they shall not touch you? and when you are thirsty, go to the vessels, and drink of that which the young men have drawn.

Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni? Ruthu 2:10

Then she fell on her face, and bowed herself to the ground, and said to him, Why have I found favor in your sight, that you should take knowledge of me, seeing I am a foreigner?

Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo. Ruthu 2:11

Boaz answered her, It has fully been shown me, all that you have done to your mother-in-law since the death of your husband; and how you have left your father and your mother, and the land of your birth, and have come to a people that you didn't know before.

Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake. Ruthu 2:12

Yahweh recompense your work, and a full reward be given you of Yahweh, the God of Israel, under whose wings you are come to take refuge.

Ndipo aliposema, Bwana wangu, na nipate kibali machoni pako; kwa sababu wewe umeniburudisha moyo, na kumwambia mema mjakazi wako, ingawa mimi si kama mmojawapo wa wajakazi wako. Ruthu 2:13

Then she said, Let me find favor in your sight, my lord, because you have comforted me, and because you have spoken kindly to your handmaid, though I am not as one of your handmaidens.

Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza. Ruthu 2:14

At meal-time Boaz said to her, Come here, and eat of the bread, and dip your morsel in the vinegar. She sat beside the reapers, and they reached her parched grain, and she ate, and was sufficed, and left of it.

Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee. Ruthu 2:15

When she was risen up to glean, Boaz commanded his young men, saying, Let her glean even among the sheaves, and don't reproach her.

Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze. Ruthu 2:16

Also pull out some for her from the bundles, and leave it, and let her glean, and don't rebuke her.

Basi Ruthuu akaokota masazo kondeni hata jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri. Ruthu 2:17

So she gleaned in the field until even; and she beat out that which she had gleaned, and it was about an ephah of barley.

Akajitwika, akaenda zake mjini. Akamwonyesha mkwewe zile alizoziokota; akavitoa vile vyakula alivyovisaza alipokwisha kushiba, akampa. Ruthu 2:18

She took it up, and went into the city; and her mother-in-law saw what she had gleaned: and she brought forth and gave to her that which she had left after she was sufficed.

Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu niliyefanya kazi kwake leo jina lake aitwa Boazi. Ruthu 2:19

Her mother-in-law said to her, Where have you gleaned today? and where have you worked? blessed be he who did take knowledge of you. She shown her mother-in-law with whom she had worked, and said, The man's name with whom I worked today is Boaz.

Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na Bwana, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu. Ruthu 2:20

Naomi said to her daughter-in-law, Blessed be he of Yahweh, who has not left off his kindness to the living and to the dead. Naomi said to her, The man is a close relative to us, one of our near kinsmen.

Naye Ruthuu Mmoabi akasema, Naam, akaniambia, Ukae papa hapa karibu na vijana wangu, hata watakapomaliza mavuno yangu yote. Ruthu 2:21

Ruth the Moabitess said, Yes, he said to me, You shall keep fast by my young men, until they have ended all my harvest.

Kisha Naomi akamwambia Ruthuu mkwewe, Mwanangu, ni vizuri wewe ufuatane na wasichana wake, wala watu wasikukute katika konde linginelo lote. Ruthu 2:22

Naomi said to Ruth her daughter-in-law, It is good, my daughter, that you go out with his maidens, and that they not meet you in any other field.

Hivyo yeye akafuatana na wasichana wake Boazi na kuokota, hata mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano pia; naye alikuwa akikaa kwa mkwewe. Ruthu 2:23

So she kept fast by the maidens of Boaz, to glean to the end of barley harvest and of wheat harvest; and she lived with her mother-in-law.