Ruthu 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ruthu 3 (Swahili) Ruth 3 (English)

Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? Ruthu 3:1

Naomi her mother-in-law said to her, My daughter, shall I not seek rest for you, that it may be well with you?

Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani. Ruthu 3:2

Now isn't Boaz our kinsman, with whose maidens you were? Behold, he winnows barley tonight in the threshing floor.

Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa. Ruthu 3:3

Wash yourself therefore, and anoint you, and put your clothing on you, and get you down to the threshing floor, but don't make yourself known to the man, until he shall have done eating and drinking.

Nayo itakuwa wakati atakapolala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya. Ruthu 3:4

It shall be, when he lies down, that you shall mark the place where he shall lie, and you shall go in, and uncover his feet, and lay you down; and he will tell you what you shall do.

Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya. Ruthu 3:5

She said to her, All that you say I will do.

Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ruthu 3:6

She went down to the threshing floor, and did according to all that her mother-in-law bade her.

Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. Ruthu 3:7

When Boaz had eaten and drunk, and his heart was merry, he went to lie down at the end of the heap of grain: and she came softly, and uncovered his feet, and laid her down.

Na ikawa usiku wa manane yule mtu akasituka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. Ruthu 3:8

It happened at midnight, that the man was afraid, and turned himself; and, behold, a woman lay at his feet.

Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthuu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. Ruthu 3:9

He said, Who are you? She answered, I am Ruth your handmaid: spread therefore your skirt over your handmaid; for you are a near kinsman.

Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na Bwana; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri. Ruthu 3:10

He said, Blessed are you by Yahweh, my daughter: you have shown more kindness in the latter end than at the beginning, inasmuch as you didn't follow young men, whether poor or rich.

Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema. Ruthu 3:11

Now, my daughter, don't be afraid; I will do to you all that you say; for all the city of my people does know that you are a worthy woman.

Tena ndiyo kweli ya kuwa mimi ni wa jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi. Ruthu 3:12

Now it is true that I am a near kinsman; however there is a kinsman nearer than I.

Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; Bwana aishivyo. Ulale wewe hata asubuhi. Ruthu 3:13

Stay this night, and it shall be in the morning, that if he will perform to you the part of a kinsman, well; let him do the kinsman's part: but if he will not do the part of a kinsman to you, then will I do the part of a kinsman to you, as Yahweh lives: lie down until the morning.

Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga. Ruthu 3:14

She lay at his feet until the morning. She rose up before one could discern another. For he said, Let it not be known that the woman came to the threshing floor.

Tena alisema, Lete hapa shela yako uliyoivaa, uishike; naye akaishika; naye akampimia vipimo sita vya shayiri akamtwika; kisha huyo mwanamke akaenda zake mjini. Ruthu 3:15

He said, Bring the mantle that is on you, and hold it; and she held it; and he measured six [measures] of barley, and laid it on her: and he went into the city.

Basi alipofika kwa mkwewe, huyo akamwuliza, Je! Mwanangu, imekuwaje? Akamwambia yote yule mtu aliyomfanyia. Ruthu 3:16

When she came to her mother-in-law, she said, Who are you, my daughter? She told her all that the man had done to her.

Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana akaniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu. Ruthu 3:17

She said, These six [measures] of barley gave he me; for he said, "Don't go empty to your mother-in-law."

Naye mkwewe akasema, Basi, mwanangu, tulia; hata utakapojua jinsi litakavyotukia jambo hili; kwa sababu mtu huyu hataridhika, asipolimaliza jambo hilo leo. Ruthu 3:18

Then said she, "Sit still, my daughter, until you know how the matter will fall; for the man will not rest, until he has finished the thing this day."