Mika 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mika 6 (Swahili) Micah 6 (English)

Basi sasa, sikieni asemavyo Bwana; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako. Mika 6:1

Listen now to what Yahweh says: "Arise, plead your case before the mountains, And let the hills hear what you have to say.

Sikieni, enyi milima, mateto ya Bwana, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana Bwana ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli. Mika 6:2

Hear, you mountains, Yahweh's controversy, And you enduring foundations of the earth; For Yahweh has a controversy with his people, And he will contend with Israel.

Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa habari gani? Shuhudieni juu yangu. Mika 6:3

My people, what have I done to you? How have I burdened you? Answer me!

Kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako. Mika 6:4

For I brought you up out of the land of Egypt, And redeemed you out of the house of bondage. I sent before you Moses, Aaron, and Miriam.

Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya Bwana. Mika 6:5

My people, remember now what Balak king of Moab devised, And what Balaam the son of Beor answered him from Shittim to Gilgal, That you may know the righteous acts of Yahweh."

Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? Mika 6:6

How shall I come before Yahweh, And bow myself before the exalted God? Shall I come before him with burnt offerings, With calves a year old?

Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? Mika 6:7

Will Yahweh be pleased with thousands of rams? With tens of thousands of rivers of oil? Shall I give my firstborn for my disobedience? The fruit of my body for the sin of my soul?

Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! Mika 6:8

He has shown you, O man, what is good. What does Yahweh require of you, but to act justly, To love mercy, and to walk humbly with your God?

Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza. Mika 6:9

Yahweh's voice calls to the city, And wisdom sees your name: "Listen to the rod, And he who appointed it.

Je! Hata sasa hazina za uovu zingalimo nyumbani mwa wabaya, na kipimo kilichopunguka, ambacho ni chukizo? Mika 6:10

Are there yet treasures of wickedness in the house of the wicked, And a short ephah{An ephah is a measure of volume, and a short ephah is made smaller than a full ephah for the purpose of cheating customers.} that is accursed?

Je! Naweza kuwa safi nami nina mizani ya udhalimu, na mfuko wa mawe ya kupimia ya udanganyifu? Mika 6:11

Shall I be pure with dishonest scales, And with a bag of deceitful weights?

Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao. Mika 6:12

Her rich men are full of violence, Her inhabitants speak lies, And their tongue is deceitful in their speech.

Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako. Mika 6:13

Therefore I also have struck you with a grievous wound. I have made you desolate because of your sins.

Utakula, lakini hutashiba; na fedheha yako itakuwa kati yako; nawe utahama, lakini hutachukua kitu salama; na hicho utakachochukua nitakitoa kwa upanga. Mika 6:14

You shall eat, but not be satisfied. Your humiliation will be in your midst. You will store up, but not save; And that which you save I will give up to the sword.

Utapanda, lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai. Mika 6:15

You will sow, but won't reap. You will tread the olives, but won't anoint yourself with oil; And crush grapes, but won't drink the wine.

Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu. Mika 6:16

For the statutes of Omri are kept, And all the works of the house of Ahab. You walk in their counsels, That I may make you a ruin, And her inhabitants a hissing; And you will bear the reproach of my people."