Mika 2 Swahili & English
Listen/Download AudioMika 2 (Swahili) | Micah 2 (English) |
---|---|
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao. Mika 2:1 |
Woe to those who devise iniquity And work evil on their beds! When the morning is light, they practice it, Because it is in the power of their hand. |
Nao hutamani mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake. Mika 2:2 |
They covet fields, and seize them; And houses, and take them away: And they oppress a man and his house, Even a man and his heritage. |
Basi Bwana asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya. Mika 2:3 |
Therefore thus says Yahweh: "Behold, I am planning against these people a disaster, From which you will not remove your necks, Neither will you walk haughtily; For it is an evil time. |
Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema, Sisi tumeangamizwa kabisa; Yeye analibadili fungu la watu wangu; Jinsi anavyoniondolea hilo! Awagawia waasi mashamba yetu. Mika 2:4 |
In that day they will take up a parable against you, And lament with a doleful lamentation, saying, 'We are utterly ruined! My people's possession is divided up. Indeed he takes it from me and assigns our fields to traitors!'" |
Kwa hiyo hutakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa Bwana. Mika 2:5 |
Therefore you will have no one who divides the land by lot in the assembly of Yahweh. |
Msitabiri, ndivyo watabirivyo; wasiyatabiri mambo haya; lawama hazikomi. Mika 2:6 |
"Don't you prophesy!" They prophesy. "Don't prophesy about these things. Disgrace won't overtake us." |
Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya Bwana imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu? Mika 2:7 |
Shall it be said, O house of Jacob: "Is the Spirit of Yahweh angry? Are these his doings? Don't my words do good to him who walks blamelessly?" |
Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita. Mika 2:8 |
But lately my people have risen up as an enemy. You strip the robe and clothing from those who pass by without a care, returning from battle. |
Wanawake wa watu wangu mwawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mwawanyang'anya utukufu wangu milele. Mika 2:9 |
You drive the women of my people out from their pleasant houses; From their young children you take away my blessing forever. |
Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo mazito sana. Mika 2:10 |
Arise, and depart! For this is not your resting place, Because of uncleanness that destroys, Even with a grievous destruction. |
Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa. Mika 2:11 |
If a man walking in a spirit of falsehood lies: 'I will prophesy to you of wine and of strong drink;' He would be the prophet of this people. |
Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia; Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli; Nitawaweka pamoja kama kondoo wa Bozra; Kama kundi la kondoo kati ya malisho yao; Watafanya mvumo kwa wingi wa watu; Mika 2:12 |
I will surely assemble, Jacob, all of you; I will surely gather the remnant of Israel; I will put them together as the sheep of Bozrah, As a flock in the midst of their pasture; They will swarm with people. |
Avunjaye amekwea juu mbele yao; Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni, Wakatoka nje huko; Mfalme wao naye amepita akiwatangulia, Naye Bwana ametangulia mbele yao. Mika 2:13 |
He who breaks open the way goes up before them. They break through the gate, and go out. And their king passes on before them, With Yahweh at their head." |