Mika 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mika 4 (Swahili) Micah 4 (English)

Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Mika 4:1

But in the latter days, It will happen that the mountain of Yahweh's temple will be established on the top of the mountains, And it will be exalted above the hills; And peoples will stream to it.

Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. Mika 4:2

Many nations will go and say, "Come, and let us go up to the mountain of Yahweh, And to the house of the God of Jacob; And he will teach us of his ways, And we will walk in his paths." For out of Zion will go forth the law, And the word of Yahweh from Jerusalem;

Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Mika 4:3

And he will judge between many peoples, And will decide concerning strong nations afar off. They will beat their swords into plowshares, And their spears into pruning hooks. Nation will not lift up sword against nation, Neither will they learn war any more.

Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi. Mika 4:4

But they will sit every man under his vine and under his fig tree; And no one will make them afraid: For the mouth of Yahweh of Hosts has spoken.

Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana, Mungu wetu, milele na milele. Mika 4:5

Indeed all the nations may walk in the name of their gods; But we will walk in the name of Yahweh our God forever and ever.

Katika siku ile, asema Bwana, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa. Mika 4:6

"In that day," says Yahweh, "I will assemble that which is lame, And I will gather that which is driven away, And that which I have afflicted;

Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na Bwana atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele. Mika 4:7

And I will make that which was lame a remnant, And that which was cast far off a strong nation: And Yahweh will reign over them on Mount Zion from then on, even forever.

Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu. Mika 4:8

You, tower of the flock, the hill of the daughter of Zion, To you it will come, Yes, the former dominion will come, The kingdom of the daughter of Jerusalem.

Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na utungu kama mwanamke wakati wa kuzaa? Mika 4:9

Now why do you cry out aloud? Is there no king in you? Has your counselor perished, That pains have taken hold of you as of a woman in travail?

Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa katika mikono ya adui zako. Mika 4:10

Be in pain, and labor to bring forth, daughter of Zion, Like a woman in travail; For now you will go forth out of the city, And will dwell in the field, And will come even to Babylon. There you will be rescued. There Yahweh will redeem you from the hand of your enemies.

Na sasa mataifa mengi wamekusanyika juu yako, wasemao, Na atiwe unajisi; macho yetu na yaone shari ya Sayuni. Mika 4:11

Now many nations have assembled against you, that say, 'Let her be defiled, And let our eye gloat over Zion.'

Lakini wao hawayajui mawazo ya Bwana, wala hawafahamu shauri lake; kwa maana amewakusanya kama miganda sakafuni. Mika 4:12

But they don't know the thoughts of Yahweh, Neither do they understand his counsel; For he has gathered them like the sheaves to the threshing floor.

Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda-ponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa Bwana, na mali zao kwa Bwana wa dunia yote. Mika 4:13

Arise and thresh, daughter of Zion; For I will make your horn iron, And I will make your hoofs brass; And you will beat in pieces many peoples: And I will devote their gain to Yahweh, And their substance to the Lord of the whole earth.