Mika 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mika 3 (Swahili) Micah 3 (English)

Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? Mika 3:1

I said, "Please listen, you heads of Jacob, And rulers of the house of Israel: Isn't it for you to know justice?

Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. Mika 3:2

You who hate the good, And love the evil; Who tear off their skin, And their flesh from off their bones;

Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani. Mika 3:3

Who also eat the flesh of my people, And flay their skin from off them, And break their bones, And chop them in pieces, as for the pot, And as flesh within the caldron.

Ndipo watakapomwomba Bwana, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao. Mika 3:4

Then they will cry to Yahweh, But he will not answer them. Yes, he will hide his face from them at that time, Because they made their deeds evil."

Bwana asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita. Mika 3:5

Thus says Yahweh concerning the prophets who lead my people astray; for those who feed their teeth, they proclaim, "Peace!" and whoever doesn't provide for their mouths, they prepare war against him:

Kwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono; tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri; nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao. Mika 3:6

"Therefore night is over you, with no vision, And it is dark to you, that you may not divine; And the sun will go down on the prophets, And the day will be black over them.

Na hao waonaji watatahayarika, na wenye kubashiri watafadhaika; naam, hao wote watajifunika midomo yao; kwa maana; hapana jawabu la Mungu. Mika 3:7

The seers shall be disappointed, And the diviners confounded. Yes, they shall all cover their lips; For there is no answer from God."

Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Mika 3:8

But as for me, I am full of power by the Spirit of Yahweh, And of judgment, and of might, To declare to Jacob his disobedience, And to Israel his sin.

Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Mika 3:9

Please listen to this, you heads of the house of Jacob, And rulers of the house of Israel, Who abhor justice, And pervert all equity.

Wanaijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Mika 3:10

They build up Zion with blood, And Jerusalem with iniquity.

Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea Bwana, na kusema, Je! Hayupo Bwana katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia. Mika 3:11

Her leaders judge for bribes, And her priests teach for a price, And her prophets of it tell forturnes for money: Yet they lean on Yahweh, and say, Isn't Yahweh in the midst of us? No disaster will come on us.

Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.

Mika 3:12

Therefore Zion for your sake will be plowed like a field, And Jerusalem will become heaps of rubble, And the mountain of the temple like the high places of a forest.