Hosea 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hosea 4 (Swahili) Hosea 4 (English)

Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hosea 4:1

Hear the word of Yahweh, you children of Israel; For Yahweh has a charge against the inhabitants of the land: "Indeed there is no truth, Nor goodness, Nor knowledge of God in the land.

Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu. Hosea 4:2

There is cursing, lying, murder, stealing, and committing adultery; They break boundaries, and bloodshed causes bloodshed.

Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa kondeni na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataondolewa. Hosea 4:3

Therefore the land will mourn, And everyone who dwells therein will waste away. All living things in her, Even the animals of the field and the birds of the sky; Yes, the fish of the sea also die.

Walakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani. Hosea 4:4

"Yet let no man bring a charge, neither let any man accuse; For your people are like those who bring charges against a priest.

Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako. Hosea 4:5

You will stumble in the day, And the prophet will also stumble with you in the night; And I will destroy your mother.

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Hosea 4:6

My people are destroyed for lack of knowledge. Because you have rejected knowledge, I will also reject you, That you may be no priest to me. Because you have your God's law, I will also forget your children.

Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi; nami nitageuza utukufu wao kuwa aibu. Hosea 4:7

As they were multiplied, so they sinned against me. I will change their glory into shame.

Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao. Hosea 4:8

They feed on the sin of my people, And set their heart on their iniquity.

Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao. Hosea 4:9

It will be, like people, like priest; And I will punish them for their ways, And will repay them for their deeds.

Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Hosea 4:10

They will eat, and not have enough. They will play the prostitute, and will not increase; Because they have abandoned giving to Yahweh.

Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu. Hosea 4:11

Prostitution, wine, and new wine take away understanding.

Watu wangu hutaka shauri kwa gongo lao, na fimbo yao huwahubiri mambo; maana roho ya uzinzi imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao. Hosea 4:12

My people consult with their wooded idol, And answer to a stick of wood. Indeed the spirit of prostitution has led them astray, And they have been unfaithful to their God.

Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza uvumba juu ya vilima, chini ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini, na bibi arusi zenu hufanya uasherati. Hosea 4:13

They sacrifice on the tops of the mountains, And burn incense on the hills, under oaks and poplars and terebinths, Because its shade is good. Therefore your daughters play the prostitute, And your brides commit adultery.

Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wao wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia. Hosea 4:14

I will not punish your daughters when they play the prostitute, Nor your brides when they commit adultery; Because the men consort with prostitutes, And they sacrifice with the shrine prostitutes; And the people that does not understand will come to ruin.

Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo Bwana. Hosea 4:15

"Though you, Israel, play the prostitute, Yet don't let Judah offend; And don't come to Gilgal, Neither go up to Beth Aven, Nor swear, 'As Yahweh lives.'

Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! Bwana atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye nafasi! Hosea 4:16

For Israel has behaved extremely stubbornly, like a stubborn heifer. Then how will Yahweh feed them like a lamb in a meadow.

Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. Hosea 4:17

Ephraim is joined to idols. Leave him alone!

Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu. Hosea 4:18

Their drink has become sour. They play the prostitute continually. Her rulers dearly love their shameful way.

Upepo umemfunikiza kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao. Hosea 4:19

The wind has wrapped her up in its wings; And they shall be disappointed because of their sacrifices.