Hosea 14 Swahili & English
Listen/Download AudioHosea 14 (Swahili) | Hosea 14 (English) |
---|---|
Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. Hosea 14:1 |
Israel, return to Yahweh your God; For you have fallen because of your sin. |
Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe. Hosea 14:2 |
Take words with you, and return to Yahweh. Tell him, "Forgive all our sins, And accept that which is good: So we offer like bulls our lips. |
Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema. Hosea 14:3 |
Assyria can't save us. We won't ride on horses; Neither will we say any more to the work of our hands, 'Our gods!' For in you the fatherless finds mercy." |
Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. Hosea 14:4 |
"I will heal their waywardness. I will love them freely; For my anger is turned away from him. |
Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni. Hosea 14:5 |
I will be like the dew to Israel. He will blossom like the lily, And send down his roots like Lebanon. |
Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni. Hosea 14:6 |
His branches will spread, And his beauty will be like the olive tree, And his fragrance like Lebanon. |
Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni. Hosea 14:7 |
Men will dwell in his shade. They will revive like the grain, And blossom like the vine. Their fragrance will be like the wine of Lebanon. |
Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako. Hosea 14:8 |
Ephraim, what have I to do any more with idols? I answer, and will take care of him. I am like a green fir tree; From me your fruit is found." |
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake. Hosea 14:9 |
Who is wise, that he may understand these things? Who is prudent, that he may know them? For the ways of Yahweh are right, And the righteous walk in them; But the rebellious stumble in them. |