Sifa Lyrics

Amenihurumia by Maggie Muliri cover art

Maggie Muliri - Amenihurumia Lyrics

Artist:
Maggie Muliri

Lyrics

Amenihurumia huyu Yesu
Amenitendea huyu Yesu
Ooh amenikumbuka huyu Yesu..

Faili langu limesomwa leo nimeshinda kesi
Faili langu limesomwa leo nimeshinda kesi
Kesi niliyohukumiwa na shetani
Kesi niliyohukumiwa na wachawi
Kesi niliyohukumiwa na wanadamu

Eeh Mungu wangu, eeh Mungu wangu
Eeh Mungu wangu, ooh Baba umenihurumia

Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi

Wanadamu wamenishtaki kwa maneno mengi
Wanadamu wamenishtaki kwa taarifa nyingi
Na wengine wamenitamkia maneno magumu
Huyu Mungu wa huruma amesimama
Huyu Mungu wa faraja amesimama

Kesi niliyohukumiwa sifai mimi
Kesi walionitabiria umasikini
Kesi walionitabiria kukataliwa
Kesi niliyohukumiwa na wanadamu

Ooh Bwana wangu Yesu, ooh Bwana wangu
Ooh Bwana wangu, ooh Bwana wangu
Umenifutia aibu yangu
Umeniondolea aibu mimi
Umefuta aibu yangu

Umenivika paji la heshima tena nimeshukuru
Umenivisha vazi ya utawala sasa ninashukuru
Umenipa sura ya kuheshimika ninashukuru

Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi
(Umeficha aibu yangu Jehovah)
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi

Niliyeitwa mlaumiwa umebadili majina yangu
Ninaitwa sawa sawa kubarikiwa
Umenihurumia 

Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana wangu
Eeh Bwana wangu, eeh Bwana umenihurumia mimi

Video