Sifa Lyrics

Msaada Wangu - Zaburi  by Geraldine Oduor cover art

Geraldine Oduor - Msaada Wangu - Zaburi Lyrics

Artist:
Geraldine Oduor

Lyrics

Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi
Msaada wangu kwako Bwana


Nakuinulia macho yangu
Wewe uketiye juu sana
Kama macho ya watumishi
Wa mkono wa Bwana zao
Nilitewe nuru yako
Kweli azidi kuniongoza
Zinifikishe kwenye mlima
Maskani yako takatifu


Bwana ndiye mlinzi wangu
Uvuli wa mkono wake
Jua halinipigi mchana

Wala mwezi usiku
Anilinda na mabaya
Atalinda nafsi yangu
Nitokapo na niingiapo
Tangu sasa na milele


Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi?
Msaada wangu kwako Bwana


Sheria yako ni kamilifu
Huiburudisha nafsi yangu
Ushuhuda wako ni amini, hunitia hekima
Maagizo yako ni adili, hufurahisha nafsi yangu
Amri yako ni safi sana, huyatia macho huru


Kilicho chako ni kitakatifu, Kinadumu milele
Hukumu zako ni za kweli, zina haki kabisa
Kuliko wengi wa dhahabu, hukumu zako zatamanika
Kuliko sega za asali, hukumu zako tamu kweli


Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi?
Msaada wangu kwako Bwana


Bass
Nitayainua macho yangu milimani
Wewe u msaada, wangu wa karibu


Video