Wafilipi BSB

Wafilipi 4

Philippians Chapter 4

1
Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Therefore, my brothers, whom I love and long for, my joy and crown, that is how you must stand firm in the Lord, my beloved.
2
Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana.
I urge Euodia and Syntyche to agree with each other in the Lord.
3
Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Yes, and I ask you, my true yokefellow, to help these women who have contended at my side for the gospel, along with Clement and the rest of my fellow workers, whose names are in the Book of Life.
4
Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice!
5
Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.
Let your gentleness be apparent to all. The Lord is near.
6
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Be anxious for nothing, but in everything, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God.
7
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
And the peace of God, which surpasses all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.
8
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Finally, brothers, whatever is true, whatever is honorable, whatever is right, whatever is pure, whatever is lovely, whatever is admirable—if anything is excellent or praiseworthy—think on these things.
9
Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
Whatever you have learned or received or heard from me, or seen in me, put it into practice. And the God of peace will be with you.
10
Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
Now I rejoice greatly in the Lord that at last you have revived your concern for me. You were indeed concerned, but you had no opportunity to show it.
11
Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.
I am not saying this out of need, for I have learned to be content regardless of my circumstances.
12
Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
I know how to live humbly, and I know how to abound. In any and every situation I have learned the secret of being filled and being hungry, of having plenty and having need.
13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
I can do all things through Christ who gives me strength.
14
Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.
Nevertheless, you have done well to share in my affliction.
15
Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
And as you Philippians know, in the early days of the gospel, when I left Macedonia, no church but you partnered with me in the matter of giving and receiving.
16
Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.
For even while I was in Thessalonica, you provided for my needs again and again.
17
Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
Not that I am seeking a gift, but I am looking for the fruit that may be credited to your account.
18
Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
I have all I need and more, now that I have received your gifts from Epaphroditus. They are a fragrant offering, an acceptable sacrifice, well-pleasing to God.
19
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
And my God will supply all your needs according to His glorious riches in Christ Jesus.
20
Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
To our God and Father be glory forever and ever. Amen.
21
Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu.
Greet all the saints in Christ Jesus. The brothers who are with me send you greetings.
22
Watakatifu wote wawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari.
All the saints send you greetings, especially those from the household of Caesar.
23
Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.
The grace of the Lord Jesus Christ be with your spirit.

Chagua Sura

1 2 3 4