Yakobo 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yakobo 5 (Swahili) James 5 (English)

Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Yakobo 5:1

Come now, you rich, weep and howl for your miseries that are coming on you.

Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Yakobo 5:2

Your riches are corrupted and your garments are moth-eaten.

Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Yakobo 5:3

Your gold and your silver are corroded, and their corrosion will be for a testimony against you, and will eat your flesh like fire. You have laid up your treasure in the last days.

Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Yakobo 5:4

Behold, the wages of the laborers who mowed your fields, which you have kept back by fraud, cry out, and the cries of those who reaped have entered into the ears of the Lord of Hosts.

Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Yakobo 5:5

You have lived delicately on the earth, and taken your pleasure. You have nourished your hearts as in a day of slaughter.

Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi. Yakobo 5:6

You have condemned, you have murdered the righteous one. He doesn't resist you.

Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Yakobo 5:7

Be patient therefore, brothers, until the coming of the Lord. Behold, the farmer waits for the precious fruit of the earth, being patient over it, until it receives the early and late rain.

Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Yakobo 5:8

You also be patient. Establish your hearts, for the coming of the Lord is at hand.

Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Yakobo 5:9

Don't grumble, brothers, against one another, so that you won't be judged. Behold, the judge stands at the door.

Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Yakobo 5:10

Take, brothers, for an example of suffering and of patience, the prophets who spoke in the name of the Lord.

Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma. Yakobo 5:11

Behold, we call them blessed who endured. You have heard of the patience of Job, and have seen the Lord in the outcome, and how the Lord is full of compassion and mercy.

Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu. Yakobo 5:12

But above all things, my brothers, don't swear, neither by heaven, nor by the earth, nor by any other oath; but let your "yes" be "yes," and your "no," "no;" so that you don't fall into hypocrisy.{TR reads "under judgment" instead of "into hypocrisy"}

Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. Yakobo 5:13

Is any among you suffering? Let him pray. Is any cheerful? Let him sing praises.

Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Yakobo 5:14

Is any among you sick? Let him call for the elders of the assembly, and let them pray over him, anointing him with oil in the name of the Lord,

Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Yakobo 5:15

and the prayer of faith will heal him who is sick, and the Lord will raise him up. If he has committed sins, he will be forgiven.

Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Yakobo 5:16

Confess your offenses to one another, and pray one for another, that you may be healed. The effective, earnest prayer of a righteous man is powerfully effective.

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Yakobo 5:17

Elijah was a man with a nature like ours, and he prayed earnestly that it might not rain, and it didn't rain on the earth for three years and six months.

Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. Yakobo 5:18

He prayed again, and the sky gave rain, and the earth brought forth its fruit.

Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; Yakobo 5:19

Brothers, if any among you wanders from the truth, and someone turns him back,

jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. Yakobo 5:20

let him know that he who turns a sinner from the error of his way will save a soul from death, and will cover a multitude of sins.