Hosea 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hosea 14 (Swahili) Hosea 14 (English)

Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. Hosea 14:1

Israel, return to Yahweh your God; For you have fallen because of your sin.

Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe. Hosea 14:2

Take words with you, and return to Yahweh. Tell him, "Forgive all our sins, And accept that which is good: So we offer like bulls our lips.

Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema. Hosea 14:3

Assyria can't save us. We won't ride on horses; Neither will we say any more to the work of our hands, 'Our gods!' For in you the fatherless finds mercy."

Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. Hosea 14:4

"I will heal their waywardness. I will love them freely; For my anger is turned away from him.

Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni. Hosea 14:5

I will be like the dew to Israel. He will blossom like the lily, And send down his roots like Lebanon.

Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni. Hosea 14:6

His branches will spread, And his beauty will be like the olive tree, And his fragrance like Lebanon.

Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni. Hosea 14:7

Men will dwell in his shade. They will revive like the grain, And blossom like the vine. Their fragrance will be like the wine of Lebanon.

Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako. Hosea 14:8

Ephraim, what have I to do any more with idols? I answer, and will take care of him. I am like a green fir tree; From me your fruit is found."

Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake. Hosea 14:9

Who is wise, that he may understand these things? Who is prudent, that he may know them? For the ways of Yahweh are right, And the righteous walk in them; But the rebellious stumble in them.