Hosea 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hosea 1 (Swahili) Hosea 1 (English)

Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beeri, siku za Uzia, na Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli. Hosea 1:1

The word of Yahweh that came to Hosea the son of Beeri, in the days of Uzziah, Jotham, Ahaz, and Hezekiah, kings of Judah, and in the days of Jeroboam the son of Joash, king of Israel.

Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana. Hosea 1:2

When Yahweh spoke at the first by Hosea, Yahweh said to Hosea, "Go, take for yourself a wife of prostitution and children of unfaithfulness; for the land commits great adultery against from Yahweh."

Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Diblaimu; naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume. Hosea 1:3

So he went and took Gomer the daughter of Diblaim; and she conceived, and bore him a son.

Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli. Hosea 1:4

Yahweh said to him, "Call his name Jezreel; for yet a little while, and I will avenge the blood of Jezreel on the house of Jehu, and will cause the kingdom of the house of Israel to cease.

Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli. Hosea 1:5

It will happen in that day that I will break the bow of Israel in the valley of Jezreel."

Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena,nisije nikawasamehe kwa njia yoyote. Hosea 1:6

She conceived again, and bore a daughter. Then he said to him, "Call her name Lo-Ruhamah{Lo-Ruhamah means "not loved."}; for I will no longer have mercy on the house of Israel, that I should in any way pardon them.

Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa Bwana, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi. Hosea 1:7

But I will have mercy on the house of Judah, and will save them by Yahweh their God, and will not save them by bow, nor by sword, nor by battle, by horses, nor by horsemen."

Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama, akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamume. Hosea 1:8

Now when she had weaned Lo-Ruhamah, she conceived, and bore a son.

Bwana akasema, Mwite jina lake Lo-ami kwa maana ninyi si watu wangu,wala mimi sitakuwa MUNGU wenu. Hosea 1:9

He said, "Call his name Lo-Ammi{Lo-Ammi means "not my people"}; for you are not my people, and I will not be yours.

Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai. Hosea 1:10

Yet the number of the children of Israel will be as the sand of the sea, which can't be measured nor numbered; and it will come to pass that, in the place where it was said to them, 'You are not my people,' they will be called 'sons of the living God.'

Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana. Hosea 1:11

The children of Judah and the children of Israel will be gathered together, and they will appoint themselves one head, and will go up from the land; for great will be the day of Jezreel.