Wagalatia 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wagalatia 5 (Swahili) Galatians 5 (English)

Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Wagalatia 5:1

Stand firm therefore in the liberty by which Christ has made us free, and don't be entangled again with a yoke of bondage.

Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Wagalatia 5:2

Behold, I, Paul, tell you that if you receive circumcision, Christ will profit you nothing.

Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Wagalatia 5:3

Yes, I testify again to every man who receives circumcision, that he is a debtor to do the whole law.

Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Wagalatia 5:4

You are alienated from Christ, you who desire to be justified by the law. You have fallen away from grace.

Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Wagalatia 5:5

For we, through the Spirit, by faith wait for the hope of righteousness.

Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo. Wagalatia 5:6

For in Christ Jesus neither circumcision amounts to anything, nor uncircumcision, but faith working through love.

Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Wagalatia 5:7

You were running well! Who interfered with you that you should not obey the truth?

Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. Wagalatia 5:8

This persuasion is not from him who calls you.

Chachu kidogo huchachua donge zima. Wagalatia 5:9

A little yeast grows through the whole lump.

Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote. Wagalatia 5:10

I have confidence toward you in the Lord that you will think no other way. But he who troubles you will bear his judgment, whoever he is.

Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika! Wagalatia 5:11

But I, brothers, if I still preach circumcision, why am I still persecuted? Then the stumbling-block of the cross has been removed.

Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao! Wagalatia 5:12

I wish that those who disturb you would cut themselves off.

Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Wagalatia 5:13

For you, brothers, were called for freedom. Only don't use your freedom for gain to the flesh, but through love be servants to one another.

Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Wagalatia 5:14

For the whole law is fulfilled in one word, in this: "You shall love your neighbor as yourself."

Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana. Wagalatia 5:15

But if you bite and devour one another, be careful that you don't consume one another.

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Wagalatia 5:16

But I say, walk by the Spirit, and you won't fulfill the lust of the flesh.

Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Wagalatia 5:17

For the flesh lusts against the Spirit, and the Spirit against the flesh; and these are contrary to one other, that you may not do the things that you desire.

Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Wagalatia 5:18

But if you are led by the Spirit, you are not under the law.

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, Wagalatia 5:19

Now the works of the flesh are obvious, which are: adultery, sexual immorality, uncleanness, lustfulness,

ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, Wagalatia 5:20

idolatry, sorcery, hatred, strife, jealousies, outbursts of anger, rivalries, divisions, heresies,

husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:21

envyings, murders, drunkenness, orgies, and things like these; of which I forewarn you, even as I also forewarned you, that those who practice such things will not inherit the Kingdom of God.

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, Wagalatia 5:22

But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faithfulness,

upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Wagalatia 5:23

gentleness, and self-control. Against such things there is no law.

Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Wagalatia 5:24

Those who belong to Christ have crucified the flesh with its passions and lusts.

Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Wagalatia 5:25

If we live by the Spirit, let's also walk by the Spirit.

Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Wagalatia 5:26

Let's not become conceited, provoking one another, and envying one another.