Wagalatia 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wagalatia 6 (Swahili) Galatians 6 (English)

Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Wagalatia 6:1

Brothers, even if a man is caught in some fault, you who are spiritual must restore such a one in a spirit of gentleness; looking to yourself so that you also aren't tempted.

Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Wagalatia 6:2

Bear one another's burdens, and so fulfill the law of Christ.

Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Wagalatia 6:3

For if a man thinks himself to be something when he is nothing, he deceives himself.

Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Wagalatia 6:4

But let each man test his own work, and then he will take pride in himself and not in his neighbor.

Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. Wagalatia 6:5

For each man will bear his own burden.

Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. Wagalatia 6:6

But let him who is taught in the word share all good things with him who teaches.

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Wagalatia 6:7

Don't be deceived. God is not mocked, for whatever a man sows, that will he also reap.

Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Wagalatia 6:8

For he who sows to his own flesh will from the flesh reap corruption. But he who sows to the Spirit will from the Spirit reap eternal life.

Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Wagalatia 6:9

Let us not be weary in doing good, for we will reap in due season, if we don't give up.

Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. Wagalatia 6:10

So then, as we have opportunity, let's do what is good toward all men, and especially toward those who are of the household of the faith.

Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe! Wagalatia 6:11

See with what large letters I write to you with my own hand.

Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu. Wagalatia 6:12

As many as desire to look good in the flesh, they compel you to be circumcised; only that they may not be persecuted for the cross of Christ.

Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. Wagalatia 6:13

For even they who receive circumcision don't keep the law themselves, but they desire to have you circumcised, that they may boast in your flesh.

Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Wagalatia 6:14

But far be it from me to boast, except in the cross of our Lord Jesus Christ, through which the world has been crucified to me, and I to the world.

Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Wagalatia 6:15

For in Christ Jesus neither is circumcision anything, nor uncircumcision, but a new creation.

Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Wagalatia 6:16

As many as walk by this rule, peace and mercy be on them, and on God's Israel.

Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. Wagalatia 6:17

From now on, let no one cause me any trouble, for I bear the marks of the Lord Jesus branded on my body.

Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina. Wagalatia 6:18

The grace of our Lord Jesus Christ be with your spirit, brothers. Amen.