Ezra 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezra 8 (Swahili) Ezra 8 (English)

Basi hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao, na hii ndiyo nasaba ya wale waliokwea pamoja nami kutoka Babeli, wakati wa kutawala kwake mfalme Artashasta. Ezra 8:1

Now these are the heads of their fathers' [houses], and this is the genealogy of those who went up with me from Babylon, in the reign of Artaxerxes the king:

Wa wana wa Finehasi, Gershoni; wa wana wa Ithamari, Danieli; wa wana wa Daudi, Hatushi, mwana wa Shekania; Ezra 8:2

Of the sons of Phinehas, Gershom. Of the sons of Ithamar, Daniel. Of the sons of David, Hattush.

wa wana wa Paroshi, Zekaria; na pamoja naye wakahesabiwa kwa nasaba wanaume mia na hamsini. Ezra 8:3

Of the sons of Shecaniah, of the sons of Parosh, Zechariah; and with him were reckoned by genealogy of the males one hundred fifty.

Wa wana wa Pahath-Moabu, Eliehoenai, mwana wa Zerahia; na pamoja naye wanaume mia mbili; Ezra 8:4

Of the sons of Pahath-moab, Eliehoenai the son of Zerahiah; and with him two hundred males.

Wa wana wa Zatu, Shekania, mwana wa Yahazieli; na pamoja naye wanaume mia tatu. Ezra 8:5

Of the sons of Shecaniah, the son of Jahaziel; and with him three hundred males.

Na wa wana wa Adini, Ebedi, mwana wa Yonathani; na pamoja naye wanaume hamsini. Ezra 8:6

Of the sons of Adin, Ebed the son of Jonathan; and with him fifty males.

Na wa wana wa Elamu, Yeshaya, mwana wa Athalia; na pamoja naye wanaume sabini. Ezra 8:7

Of the sons of Elam, Jeshaiah the son of Athaliah; and with him seventy males.

Na wa wana wa Shefatia, Zebadia, mwana wa Mikaeli; na pamoja naye wanaume themanini. Ezra 8:8

Of the sons of Shephatiah, Zebadiah the son of Michael; and with him eighty males.

Wa wana wa Yoabu, Obadia, mwana wa Yehieli; na pamoja naye wanaume mia mbili na kumi na wanane. Ezra 8:9

Of the sons of Joab, Obadiah the son of Jehiel; and with him two hundred and eighteen males.

Na wa wana wa Binui, Shelomithi, mwana wa Yosifia; na pamoja naye wanaume mia na sitini. Ezra 8:10

Of the sons of Shelomith, the son of Josiphiah; and with him one hundred sixty males.

Na wa wana wa Bebai, Zekaria, mwana wa Bebai; na pamoja naye wanaume ishirini na wanane. Ezra 8:11

Of the sons of Bebai, Zechariah the son of Bebai; and with him twenty-eight males.

Na wa wana wa Azgadi, Yohana, mwana wa Hakatani; na pamoja naye wanaume mia na kumi. Ezra 8:12

Of the sons of Azgad, Johanan the son of Hakkatan; and with him one hundred ten males.

Na wa wana wa Adonikamu, hawa waliokuwa wa mwisho, na hayo ndiyo majina yao, Elifeleti, na Yeueli, na Shemaya; na pamoja nao wanaume sitini. Ezra 8:13

Of the sons of Adonikam, [who were] the last; and these are their names: Eliphelet, Jeuel, and Shemaiah; and with them sixty males.

Na wa wana wa Bigwai, Uthai, mwana wa Zabudi; na pamoja naye wanaume sabini. Ezra 8:14

Of the sons of Bigvai, Uthai and Zabbud; and with them seventy males.

Nikawakusanya penye mto ushukao kwenda Ahava; na huko tukapiga kambi yetu muda wa siku tatu; nikawakagua watu, na makuhani, wala sikuona hapo wana wa Lawi hata mmoja. Ezra 8:15

I gathered them together to the river that runs to Ahava; and there we encamped three days: and I viewed the people, and the priests, and found there none of the sons of Levi.

Ndipo nikatuma watu kwenda kumwita Eliezeri, na Arieli, na Shemaya, na Elnathani, na Yaribu, na Elnathani, na Nathani, na Zekaria, na Meshulamu, waliokuwa wakuu; na Yoyaribu, na Elnathani pia, waliokuwa waalimu. Ezra 8:16

Then sent I for Eliezer, for Ariel, for Shemaiah, and for Elnathan, and for Jarib, and for Elnathan, and for Nathan, and for Zechariah, and for Meshullam, chief men; also for Joiarib, and for Elnathan, who were teachers.

Nikawapeleka kwa Ido, mkuu, huko Kasifia; nikawaambia watakayomwambia Ido, na ndugu zake hao Wanethini, huko Kasifia, kwamba watuletee watu watakaohudumu katika nyumba ya Mungu wetu. Ezra 8:17

I sent them forth to Iddo the chief at the place Casiphia; and I told them what they should tell Iddo, [and] his brothers the Nethinim, at the place Casiphia, that they should bring to us ministers for the house of our God.

Na kama mkono mwema wa Mungu wetu ulivyokuwa pamoja nasi, wakamletea Ishekeli, mmoja wa wana wa Mali ,mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;na Sherebia ,pamoja na wanawe na ndugu zake ,watu kumi na wanawe. Ezra 8:18

According to the good hand of our God on us they brought us a man of discretion, of the sons of Mahli, the son of Levi, the son of Israel; and Sherebiah, with his sons and his brothers, eighteen;

na Hashabia, na pamoja naye Yeshaya, wa wana wa Merari, na ndugu zake na wana wao, watu ishirini; Ezra 8:19

and Hashabiah, and with him Jeshaiah of the sons of Merari, his brothers and their sons, twenty;

na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao. Ezra 8:20

and of the Nethinim, whom David and the princes had given for the service of the Levites, two hundred and twenty Nethinim: all of them were mentioned by name.

Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote. Ezra 8:21

Then I proclaimed a fast there, at the river Ahava, that we might humble ourselves before our God, to seek of him a straight way for us, and for our little ones, and for all our substance.

Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao. Ezra 8:22

For I was ashamed to ask of the king a band of soldiers and horsemen to help us against the enemy in the way, because we had spoken to the king, saying, The hand of our God is on all those who seek him, for good; but his power and his wrath is against all those who forsake him.

Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali. Ezra 8:23

So we fasted and begged our God for this: and he was entreated of us.

Ndipo nikawatenga watu kumi na wawili wa wakuu wa makuhani, nao ni Sherebia, na Hashabia, na watu kumi wa ndugu zao pamoja nao, Ezra 8:24

Then I set apart twelve of the chiefs of the priests, even Sherebiah, Hashabiah, and ten of their brothers with them,

nami nikawapimia kwa mizani zile fedha, na dhahabu, na vile vyombo, matoleo kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu, ambayo mfalme, na washauri wake, na wakuu wake, na Israeli wote waliokuwapo, walikuwa wameyatoa; Ezra 8:25

and weighed to them the silver, and the gold, and the vessels, even the offering for the house of our God, which the king, and his counselors, and his princes, and all Israel there present, had offered:

nami nikawapimia mikononi mwao talanta za fedha mia sita na hamsini na vyombo vya fedha talanta mia; na talanta mia za dhahabu; Ezra 8:26

I weighed into their hand six hundred fifty talents of silver, and silver vessels one hundred talents; of gold one hundred talents;

na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong'aa, thamani yake sawa na dhahabu. Ezra 8:27

and twenty bowls of gold, of one thousand darics; and two vessels of fine bright brass, precious as gold.

Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa Bwana, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu. Ezra 8:28

I said to them, You are holy to Yahweh, and the vessels are holy; and the silver and the gold are a freewill-offering to Yahweh, the God of your fathers.

Basi, angalieni, na kuvitunza vitu hivi, hata mtakapovipima mbele ya wakuu wa makuhani, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa wa Israeli, huko Yerusalemu, katika vyumba vya nyumba ya Bwana. Ezra 8:29

Watch you, and keep them, until you weigh them before the chiefs of the priests and the Levites, and the princes of the fathers' [houses] of Israel, at Jerusalem, in the chambers of the house of Yahweh.

Hivyo makuhani na Walawi wakaupokea uzani wa fedha, na dhahabu, na vyombo, ili kuvileta Yerusalemu nyumbani kwa Mungu wetu. Ezra 8:30

So the priests and the Levites received the weight of the silver and the gold, and the vessels, to bring them to Jerusalem to the house of our God.

Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani. Ezra 8:31

Then we departed from the river Ahava on the twelfth [day] of the first month, to go to Jerusalem: and the hand of our God was on us, and he delivered us from the hand of the enemy and the bandit by the way.

Tukafika Yerusalemu, tukakaa huko muda wa siku tatu. Ezra 8:32

We came to Jerusalem, and abode there three days.

Hata siku ya nne, hizo fedha na dhahabu na vile vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu, vikatiwa mikononi mwa Meremothi, mwana wa Uria, kuhani; na pamoja naye alikuwapo Eleazari, mwana wa Finehasi; na pamoja nao Yozabadi, mwana wa Yeshua, na Noadia, mwana wa Binui, Walawi; Ezra 8:33

On the fourth day the silver and the gold and the vessels were weighed in the house of our God into the hand of Meremoth the son of Uriah the priest; and with him was Eleazar the son of Phinehas; and with them was Jozabad the son of Jeshua, and Noadiah the son of Binnui, the Levite;

vile vyombo vyote kwa hesabu na kwa uzani; tena uzani wake wote uliandikwa wakati ule. Ezra 8:34

the whole by number and by weight: and all the weight was written at that time.

Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo waume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. Ezra 8:35

The children of the captivity, who had come out of exile, offered burnt offerings to the God of Israel, twelve bulls for all Israel, ninety-six rams, seventy-seven lambs, and twelve male goats for a sin-offering: all this was a burnt offering to Yahweh.

Wakawapa manaibu wa mfalme, na maliwali wa ng'ambo ya Mto, maagizo ya mfalme; nao wakawapa watu, na nyumba ya Mungu, msaada. Ezra 8:36

They delivered the king's commissions to the king's satraps, and to the governors beyond the River: and they furthered the people and the house of God.