Ezra 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezra 6 (Swahili) Ezra 6 (English)

Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli. Ezra 6:1

Then Darius the king made a decree, and search was made in the house of the archives, where the treasures were laid up in Babylon.

Na chuo kimoja kilipatikana huko Akmetha, katika nyumba ya mfalme iliyo katika wilaya ya Umedi, na ndani yake maneno haya yameandikwa ili yakumbukwe. Ezra 6:2

There was found at Achmetha, in the palace that is in the province of Media, a scroll, and therein was thus written for a record:

Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini; Ezra 6:3

In the first year of Cyrus the king, Cyrus the king made a decree: Concerning the house of God at Jerusalem, let the house be built, the place where they offer sacrifices, and let the foundations of it be strongly laid; the height of it sixty cubits, and the breadth of it sixty cubits;

ziwepo safu tatu za mawe makubwa, na safu moja ya miti mipya; gharama zake zitolewe katika nyumba ya mfalme. Ezra 6:4

with three courses of great stones, and a course of new timber: and let the expenses be given out of the king's house.

Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, ambavyo mfalme Nebukadreza alivitoa katika nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu, akavileta mpaka Babeli, na virudishwe, vikaingizwe tena katika hekalu lililoko Yerusalemu, kila kimoja mahali pake, na wewe uvitie katika nyumba ya Mungu. Ezra 6:5

Also let the gold and silver vessels of the house of God, which Nebuchadnezzar took forth out of the temple which is at Jerusalem, and brought to Babylon, be restored, and brought again to the temple which is at Jerusalem, everyone to its place; and you shall put them in the house of God.

Basi sasa ninyi, Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng'ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale; Ezra 6:6

Now therefore, Tattenai, governor beyond the River, Shetharbozenai, and your companions the Apharsachites, who are beyond the River, be you far from there:

iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Ezra 6:7

let the work of this house of God alone; let the governor of the Jews and the elders of the Jews build this house of God in its place.

Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng'ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Ezra 6:8

Moreover I make a decree what you shall do to these elders of the Jews for the building of this house of God: that of the king's goods, even of the tribute beyond the River, expenses be given with all diligence to these men, that they be not hindered.

Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa; Ezra 6:9

That which they have need of, both young bulls, and rams, and lambs, for burnt offerings to the God of heaven; [also] wheat, salt, wine, and oil, according to the word of the priests who are at Jerusalem, let it be given them day by day without fail;

wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima. Ezra 6:10

that they may offer sacrifices of sweet savor to the God of heaven, and pray for the life of the king, and of his sons.

Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili. Ezra 6:11

Also I have made a decree, that whoever shall alter this word, let a beam be pulled out from his house, and let him be lifted up and fastened thereon; and let his house be made a dunghill for this:

Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. Ezra 6:12

and the God who has caused his name to dwell there overthrow all kings and peoples who shall put forth their hand to alter [the same], to destroy this house of God which is at Jerusalem. I Darius have made a decree; let it be done with all diligence.

Ndipo Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao. Ezra 6:13

Then Tattenai, the governor beyond the River, Shetharbozenai, and their companions, because that Darius the king had sent, did accordingly with all diligence.

Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi. Ezra 6:14

The elders of the Jews built and prospered, through the prophesying of Haggai the prophet and Zechariah the son of Iddo. They built and finished it, according to the commandment of the God of Israel, and according to the decree of Cyrus, and Darius, and Artaxerxes king of Persia.

Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario. Ezra 6:15

This house was finished on the third day of the month Adar, which was in the sixth year of the reign of Darius the king.

Na wana wa Israeli, na makuhani na Walawi, na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha. Ezra 6:16

The children of Israel, the priests, and the Levites, and the rest of the children of the captivity, kept the dedication of this house of God with joy.

Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng'ombe mia, na kondoo waume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli wote, kwa hesabu ya kabila za Israeli. Ezra 6:17

They offered at the dedication of this house of God one hundred bulls, two hundred rams, four hundred lambs; and for a sin-offering for all Israel, twelve male goats, according to the number of the tribes of Israel.

Wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; vile vile kama vilivyoandikwa katika chuo cha Musa. Ezra 6:18

They set the priests in their divisions, and the Levites in their courses, for the service of God, which is at Jerusalem; as it is written in the book of Moses.

Kisha, wana wa uhamisho wakaifanya Pasaka, mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi. Ezra 6:19

The children of the captivity kept the Passover on the fourteenth [day] of the first month.

Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja Pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao. Ezra 6:20

For the priests and the Levites had purified themselves together; all of them were pure: and they killed the Passover for all the children of the captivity, and for their brothers the priests, and for themselves.

Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kuitoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka Bwana, Mungu wa Israeli, Ezra 6:21

The children of Israel who had come again out of the captivity, and all such as had separated themselves to them from the filthiness of the nations of the land, to seek Yahweh, the God of Israel, ate,

wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa Bwana amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaelekee, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli. Ezra 6:22

and kept the feast of unleavened bread seven days with joy: for Yahweh had made them joyful, and had turned the heart of the king of Assyria to them, to strengthen their hands in the work of the house of God, the God of Israel.