Ezra 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezra 7 (Swahili) Ezra 7 (English)

Ikawa baada ya mambo hayo, wakati wa kutawala kwake Artashasta, mfalme wa Uajemi, Ezra, mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia, Ezra 7:1

Now after these things, in the reign of Artaxerxes king of Persia, Ezra the son of Seraiah, the son of Azariah, the son of Hilkiah,

mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu, Ezra 7:2

the son of Shallum, the son of Zadok, the son of Ahitub,

mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi, Ezra 7:3

the son of Amariah, the son of Azariah, the son of Meraioth,

mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki, Ezra 7:4

the son of Zerahiah, the son of Uzzi, the son of Bukki,

mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu; Ezra 7:5

the son of Abishua, the son of Phinehas, the son of Eleazar, the son of Aaron the chief priest;

huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa Bwana, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa Bwana, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye. Ezra 7:6

this Ezra went up from Babylon: and he was a ready scribe in the law of Moses, which Yahweh, the God of Israel, had given; and the king granted him all his request, according to the hand of Yahweh his God on him.

Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta. Ezra 7:7

There went up some of the children of Israel, and of the priests, and the Levites, and the singers, and the porters, and the Nethinim, to Jerusalem, in the seventh year of Artaxerxes the king.

Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme. Ezra 7:8

He came to Jerusalem in the fifth month, which was in the seventh year of the king.

Maana alianza kukwea kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akafika Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kama mkono mwema wa Mungu wake ulivyokuwa pamoja naye. Ezra 7:9

For on the first [day] of the first month began he to go up from Babylon; and on the first [day] of the fifth month came he to Jerusalem, according to the good hand of his God on him.

Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli. Ezra 7:10

For Ezra had set his heart to seek the law of Yahweh, and to do it, and to teach in Israel statutes and ordinances.

Basi hii ndiyo nakala ya waraka, mfalme Artashasta aliyompa Ezra, kuhani, mwandishi, naam, mwandishi wa maneno ya amri za Bwana, na wa sheria zake alizowapa Israeli. Ezra 7:11

Now this is the copy of the letter that the king Artaxerxes gave to Ezra the priest, the scribe, even the scribe of the words of the commandments of Yahweh, and of his statutes to Israel:

Artashasta, mfalme wa wafalme, kwa Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, salamu kamili; wakadhalika. Ezra 7:12

Artaxerxes, king of kings, to Ezra the priest, the scribe of the law of the God of heaven, perfect and so forth.

Natoa amri ya kwamba wote walio wa watu wa Israeli, na makuhani wao, na Walawi, katika ufalme wangu, wenye nia ya kwenda Yerusalemu kwa hiari yao wenyewe, waende pamoja nawe. Ezra 7:13

I make a decree, that all those of the people of Israel, and their priests and the Levites, in my realm, who are minded of their own free will to go to Jerusalem, go with you.

Kwa kuwa umetumwa na mfalme, na washauri wake saba, ili kuuliza habari za Yuda na Yerusalemu, kwa sheria ya Mungu wako iliyo mkononi mwako; Ezra 7:14

Because you are sent of the king and his seven counselors, to inquire concerning Judah and Jerusalem, according to the law of your God which is in your hand,

na kuichukua fedha na dhahabu, ambayo mfalme, na washauri wake, kwa hiari yao, wamemtolea Mungu wa Israeli, akaaye Yerusalemu; Ezra 7:15

and to carry the silver and gold, which the king and his counselors have freely offered to the God of Israel, whose habitation is in Jerusalem,

na fedha yote na dhahabu utakayoona katika wilaya ya Babeli, pamoja na vitu watakavyotoa watu kwa hiari yao, na vitu vya makuhani walivyotoa kwa hiari yao, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wao iliyoko Yerusalemu. Ezra 7:16

and all the silver and gold that you shall find in all the province of Babylon, with the freewill-offering of the people, and of the priests, offering willingly for the house of their God which is in Jerusalem;

Kwa sababu hiyo ujitahidi kununua kwa fedha hiyo mafahali, kondoo waume, wana-kondoo, pamoja na sadaka zao za unga, na sadaka zao za kinywaji; nawe utazitoa juu ya madhabahu ya nyumba ya Mungu wenu, iliyoko Yerusalemu. Ezra 7:17

therefore you shall with all diligence buy with this money bulls, rams, lambs, with their meal-offerings and their drink-offerings, and shall offer them on the altar of the house of your God which is in Jerusalem.

Na neno lo lote mtakaloona vema kulitenda, wewe na ndugu zako, kwa ile fedha na dhahabu itakayobaki, hilo litendeni, kama apendavyo Mungu wenu. Ezra 7:18

Whatever shall seem good to you and to your brothers to do with the rest of the silver and the gold, that do you after the will of your God.

Na vile vyombo upewavyo kwa huduma ya nyumba ya Mungu wako, virejeze mbele za Mungu wa Yerusalemu. Ezra 7:19

The vessels that are given you for the service of the house of your God, deliver you before the God of Jerusalem.

Na cho chote kitakachohitajiwa zaidi, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wako, kitakachokupasa kukitoa, kitoe katika nyumba ya hazina ya mfalme. Ezra 7:20

Whatever more shall be needful for the house of your God, which you shall have occasion to bestow, bestow it out of the king's treasure-house.

Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi, Ezra 7:21

I, even I Artaxerxes the king, do make a decree to all the treasurers who are beyond the River, that whatever Ezra the priest, the scribe of the law of the God of heaven, shall require of you, it be done with all diligence,

hata kiasi cha talanta mia za fedha, na vipimo mia vya ngano, na bathi mia za divai, na bathi mia za mafuta, na chumvi bila kuuliza kiasi chake. Ezra 7:22

to one hundred talents of silver, and to one hundred measures of wheat, and to one hundred baths of wine, and to one hundred baths of oil, and salt without prescribing how much.

Kila neno litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa mbinguni. Kwa nini itokee ghadhabu juu ya ufalme wa mfalme na wanawe? Ezra 7:23

Whatever is commanded by the God of heaven, let it be done exactly for the house of the God of heaven; for why should there be wrath against the realm of the king and his sons?

Tena twawaarifuni ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru. Ezra 7:24

Also we inform you, that touching any of the priests and Levites, the singers, porters, Nethinim, or servants of this house of God, it shall not be lawful to impose tribute, custom, or toll, on them.

Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke waamuzi na makadhi, watakaowahukumu watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; ukamfundishe yeye asiyezijua. Ezra 7:25

You, Ezra, after the wisdom of your God who is in your hand, appoint magistrates and judges, who may judge all the people who are beyond the River, all such as know the laws of your God; and teach you him who doesn't know them.

Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kwa bidii, kwamba ni kuuawa, au kwamba ni kuhamishwa, au kuondolewa mali yake, au kufungwa. Ezra 7:26

Whoever will not do the law of your God, and the law of the king, let judgment be executed on him with all diligence, whether it be to death, or to banishment, or to confiscation of goods, or to imprisonment.

Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu. Ezra 7:27

Blessed be Yahweh, the God of our fathers, who has put such a thing as this in the king's heart, to beautify the house of Yahweh which is in Jerusalem;

Naye amenifikilizia rehema zake mbele ya mfalme, na washauri wake, na mbele ya wakuu wote wa mfalme wenye mamlaka. Nami nikatiwa nguvu, kwa kadiri mkono wa Bwana, Mungu wangu, ulivyokuwa pamoja nami, nikawakusanya wakuu wote katika Israeli, ili wakwee pamoja nami.

Ezra 7:28

and has extended loving kindness to me before the king, and his counselors, and before all the king's mighty princes. I was strengthened according to the hand of Yahweh my God on me, and I gathered together out of Israel chief men to go up with me.