Wakolosai 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wakolosai 2 (Swahili) Colossians 2 (English)

Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili; Wakolosai 2:1

For I desire to have you know how greatly I struggle for you, and for those at Laodicea, and for as many as have not seen my face in the flesh;

ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; Wakolosai 2:2

that their hearts may be comforted, they being knit together in love, and gaining all riches of the full assurance of understanding, that they may know the mystery of God, both of the Father and of Christ,

ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika. Wakolosai 2:3

in whom are all the treasures of wisdom and knowledge hidden.

Nasema neno hili, mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi. Wakolosai 2:4

Now this I say that no one may delude you with persuasiveness of speech.

Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo. Wakolosai 2:5

For though I am absent in the flesh, yet am I with you in the spirit, rejoicing and seeing your order, and the steadfastness of your faith in Christ.

Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; Wakolosai 2:6

As therefore you received Christ Jesus, the Lord, walk in him,

wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. Wakolosai 2:7

rooted and built up in him, and established in the faith, even as you were taught, abounding in it in thanksgiving.

Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo. Wakolosai 2:8

Be careful that you don't let anyone rob you through his philosophy and vain deceit, after the tradition of men, after the elements of the world, and not after Christ.

Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Wakolosai 2:9

For in him all the fullness of the Godhead dwells bodily,

Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. Wakolosai 2:10

and in him you are made full, who is the head of all principality and power;

Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. Wakolosai 2:11

in whom you were also circumcised with a circumcision not made with hands, in the putting off of the body of the sins of the flesh, in the circumcision of Christ;

Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Wakolosai 2:12

having been buried with him in baptism, in which you were also raised with him through faith in the working of God, who raised him from the dead.

Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; Wakolosai 2:13

You were dead through your trespasses and the uncircumcision of your flesh. He made you alive together with him, having forgiven us all our trespasses,

akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; Wakolosai 2:14

wiping out the handwriting in ordinances which was against us; and he has taken it out of the way, nailing it to the cross;

akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. Wakolosai 2:15

having stripped the principalities and the powers, he made a show of them openly, triumphing over them in it.

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; Wakolosai 2:16

Let no man therefore judge you in eating, or in drinking, or with respect to a feast day or a new moon or a Sabbath day,

mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. Wakolosai 2:17

which are a shadow of the things to come; but the body is Christ's.

Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; Wakolosai 2:18

Let no one rob you of your prize by a voluntary humility and worshipping of the angels, dwelling in the things which he has not seen, vainly puffed up by his fleshly mind,

wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu. Wakolosai 2:19

and not holding firmly to the Head, from whom all the body, being supplied and knit together through the joints and ligaments, grows with God's growth.

Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Wakolosai 2:20

If you died with Christ from the elements of the world, why, as though living in the world, do you subject yourselves to ordinances,

Msishike, msionje, msiguse; Wakolosai 2:21

"Don't handle, nor taste, nor touch"

(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Wakolosai 2:22

(all of which perish with use), according to the precepts and doctrines of men?

Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili. Wakolosai 2:23

Which things indeed appear like wisdom in self-imposed worship, and humility, and severity to the body; but aren't of any value against the indulgence of the flesh.