Wakolosai 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wakolosai 1 (Swahili) Colossians 1 (English)

Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, Wakolosai 1:1

Paul, an apostle of Christ Jesus through the will of God, and Timothy our brother,

kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu. Wakolosai 1:2

to the saints and faithful brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} in Christ at Colossae: Grace to you and peace from God our Father, and the Lord Jesus Christ.

Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; Wakolosai 1:3

We give thanks to God the Father of our Lord Jesus Christ, praying always for you,

tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; Wakolosai 1:4

having heard of your faith in Christ Jesus, and of the love which you have toward all the saints,

kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; Wakolosai 1:5

because of the hope which is laid up for you in the heavens, of which you heard before in the word of the truth of the Gospel,

iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; Wakolosai 1:6

which has come to you; even as it is in all the world and is bearing fruit and growing, as it does in you also, since the day you heard and knew the grace of God in truth;

kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu; Wakolosai 1:7

even as you learned of Epaphras our beloved fellow servant, who is a faithful minister of Christ on our behalf,

naye alitueleza upendo wenu katika Roho. Wakolosai 1:8

who also declared to us your love in the Spirit.

Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; Wakolosai 1:9

For this cause, we also, since the day we heard this, don't cease praying and making requests for you, that you may be filled with the knowledge of his will in all spiritual wisdom and understanding,

mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; Wakolosai 1:10

that you may walk worthily of the Lord, to please him in all respects, bearing fruit in every good work, and increasing in the knowledge of God;

mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; Wakolosai 1:11

strengthened with all power, according to the might of his glory, for all endurance and perseverance with joy;

mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Wakolosai 1:12

giving thanks to the Father, who made us fit to be partakers of the inheritance of the saints in light;

Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; Wakolosai 1:13

who delivered us out of the power of darkness, and translated us into the Kingdom of the Son of his love;

ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; Wakolosai 1:14

in whom we have our redemption,{TR adds "through his blood,"} the forgiveness of our sins;

naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Wakolosai 1:15

who is the image of the invisible God, the firstborn of all creation.

Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Wakolosai 1:16

For by him were all things created, in the heavens and on the earth, things visible and things invisible, whether thrones or dominions or principalities or powers; all things have been created through him, and for him.

Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Wakolosai 1:17

He is before all things, and in him all things are held together.

Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Wakolosai 1:18

He is the head of the body, the assembly, who is the beginning, the firstborn from the dead; that in all things he might have the preeminence.

Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; Wakolosai 1:19

For all the fullness was pleased to dwell in him;

na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. Wakolosai 1:20

and through him to reconcile all things to himself, by him, whether things on the earth, or things in the heavens, having made peace through the blood of his cross.

Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; Wakolosai 1:21

You, being in past times alienated and enemies in your mind in your evil works,

katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; Wakolosai 1:22

yet now he has reconciled in the body of his flesh through death, to present you holy and without blemish and blameless before him,

mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake. Wakolosai 1:23

if it is so that you continue in the faith, grounded and steadfast, and not moved away from the hope of the Gospel which you heard, which is being proclaimed in all creation under heaven; of which I, Paul, was made a servant.

Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; Wakolosai 1:24

Now I rejoice in my sufferings for your sake, and fill up on my part that which is lacking of the afflictions of Christ in my flesh for his body's sake, which is the assembly;

ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; Wakolosai 1:25

of which I was made a servant, according to the stewardship of God which was given me toward you, to fulfill the word of God,

siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; Wakolosai 1:26

the mystery which has been hidden for ages and generations. But now it has been revealed to his saints,

ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu Wakolosai 1:27

to whom God was pleased to make known what are the riches of the glory of this mystery among the Gentiles, which is Christ in you, the hope of glory;

ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. Wakolosai 1:28

whom we proclaim, admonishing every man and teaching every man in all wisdom, that we may present every man perfect in Christ Jesus;

Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu. Wakolosai 1:29

for which I also labor, striving according to his working, which works in me mightily.