Amosi 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Amosi 7 (Swahili) Amos 7 (English)

Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme. Amosi 7:1

Thus the Lord Yahweh showed me: and, behold, he formed locusts in the beginning of the shooting up of the latter growth; and, behold, it was the latter growth after the king's harvest.

Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo. Amosi 7:2

It happened that, when they made an end of eating the grass of the land, then I said, "Lord Yahweh, forgive, I beg you! How could Jacob stand? For he is small."

Bwana akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana. Amosi 7:3

Yahweh relented concerning this. "It shall not be," says Yahweh.

Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukavila vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu. Amosi 7:4

Thus the Lord Yahweh showed me and, behold, the Lord Yahweh called for judgment by fire; and it dried up the great deep, and would have devoured the land.

Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo. Amosi 7:5

Then I said, "Lord Yahweh, stop, I beg you! How could Jacob stand? For he is small."

Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU. Amosi 7:6

Yahweh relented concerning this. "This also shall not be," says the Lord Yahweh.

Haya ndiyo aliyonionyesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake. Amosi 7:7

Thus he showed me and, behold, the Lord stood beside a wall made by a plumb line, with a plumb line in his hand.

Bwana akaniambia, Amosii, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe; Amosi 7:8

Yahweh said to me, "Amos, what do you see?" I said, "A plumb line." Then the Lord said, "Behold, I will set a plumb line in the midst of my people Israel. I will not again pass by them any more.

na mahali palipoinuka pa Isaka patakuwa ukiwa, na mahali patakatifu pa Israeli pataharibika; nami nitaondoka nishindane na nyumba ya Yeroboamu kwa upanga. Amosi 7:9

The high places of Isaac will be desolate, the sanctuaries of Israel will be laid waste; and I will rise against the house of Jeroboam with the sword."

Ndipo Amazia, kuhani wa Betheli, akapeleka habari kwa Yeroboamu, mfalme wa Israeli, akisema, Amosii amefanya fitina juu yako kati ya nyumba ya Israeli; nchi haiwezi kustahimili maneno yake yote. Amosi 7:10

Then Amaziah the priest of Beth El sent to Jeroboam king of Israel, saying, "Amos has conspired against you in the midst of the house of Israel. The land is not able to bear all his words.

Kwa maana Amosii asema hivi, Yeroboamu atakufa kwa upanga, na bila shaka Israeli atachukuliwa mbali, hali ya kufungwa, atoke katika nchi yake. Amosi 7:11

For Amos says, 'Jeroboam will die by the sword, and Israel shall surely be led away captive out of his land.'"

Tena Amazia akamwambia Amosii, Ewe mwonaji, nenda zako, ikimbilie nchi ya Yuda, ukale mkate huko, ukatabiri huko; Amosi 7:12

Amaziah also said to Amos, "You seer, go, flee away into the land of Judah, and there eat bread, and prophesy there:

lakini usitabiri tena huku Betheli; kwa maana ni mahali patakatifu pa mfalme, nayo ni nyumba ya kifalme. Amosi 7:13

but don't prophesy again any more at Bethel; for it is the king's sanctuary, and it is a royal house!"

Ndipo Amosii akajibu akamwambia Amazia, Mimi sikuwa nabii, wala sikuwa mwana wa nabii; bali nalikuwa mchungaji, na mtunza mikuyu; Amosi 7:14

Then Amos answered Amaziah, "I was no prophet, neither was I a prophet's son; but I was a herdsman, and a farmer of sycamore trees;

naye Bwana akanitwaa, katika kufuatana na kundi; Bwana akaniambia, Enenda uwatabirie watu wangu Israeli. Amosi 7:15

and Yahweh took me from following the flock, and Yahweh said to me, 'Go, prophesy to my people Israel.'

Basi, sasa lisikie neno la Bwana; Wewe unasema, Usitabiri juu ya Israeli, wala usitoe neno lako juu ya nyumba ya Isaka; Amosi 7:16

Now therefore listen to the word of Yahweh: 'You say, Don't prophesy against Israel, and don't preach against the house of Isaac.'

kwa hiyo, Bwana asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atachukuliwa mbali hali ya kufungwa kutoka nchi yake. Amosi 7:17

Therefore thus says Yahweh: 'Your wife shall be a prostitute in the city, and your sons and your daughters shall fall by the sword, and your land shall be divided by line; and you yourself shall die in a land that is unclean, and Israel shall surely be led away captive out of his land.'"