Amosi 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Amosi 3 (Swahili) Amos 3 (English)

Lisikieni neno hili alilolisema Bwana juu yenu, enyi wana wa Israeli, juu ya jamaa yote niliowapandisha kutoka nchi ya Misri, nikisema, Amosi 3:1

Hear this word that Yahweh has spoken against you, children of Israel, against the whole family which I brought up out of the land of Egypt, saying:

Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote. Amosi 3:2

"You only have I chosen of all the families of the earth. Therefore I will punish you for all of your sins."

Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Amosi 3:3

Do two walk together, Unless they have agreed?

Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwana-simba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu? Amosi 3:4

Will a lion roar in the thicket, When he has no prey? Does a young lion cry out of his den, If he has caught nothing?

Je! Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka juu ya nchi, bila kunasa kitu cho chote? Amosi 3:5

Can a bird fall in a trap on the earth, Where no snare is set for him? Does a snare spring up from the ground, When there is nothing to catch?

Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta Bwana? Amosi 3:6

Does the trumpet alarm sound in a city, Without the people being afraid? Does evil happen to a city, And Yahweh hasn't done it?

Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Amosi 3:7

Surely the Lord Yahweh will do nothing, Unless he reveals his secret to his servants the prophets.

Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri? Amosi 3:8

The lion has roared. Who will not fear? The Lord Yahweh has spoken. Who can but prophesy?

Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake. Amosi 3:9

Proclaim in the palaces at Ashdod, And in the palaces in the land of Egypt, And say, "Assemble yourselves on the mountains of Samaria, And see what unrest is in her, And what oppression is among them."

Kwa maana hawajui kutenda haki, asema Bwana, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao. Amosi 3:10

"Indeed they don't know to do right," says Yahweh, "Who hoard plunder and loot in their palaces."

Basi, haya ndiyo asemayo Bwana MUNGU; Atakuwako adui, kuizunguka nchi pande zote; naye atazishusha chini nguvu zako zikutoke; na majumba yako yatatekwa nyara. Amosi 3:11

Therefore thus says the Lord Yahweh: "An adversary will overrun the land; And he will pull down your strongholds, And your fortresses will be plundered."

Haya ndiyo asemayo Bwana; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya semadari, na juu ya mito ya hariri ya kitanda. Amosi 3:12

Thus says Yahweh: "As the shepherd rescues out of the mouth of the lion two legs, Or a piece of an ear, So shall the children of Israel be rescued who sit in Samaria on the corner of a couch, And on the silken cushions of a bed."

Sikieni, mkashuhudu juu ya nyumba ya Yakobo, asema Bwana, MUNGU wa majeshi. Amosi 3:13

"Listen, and testify against the house of Jacob," says the Lord Yahweh, the God of hosts.

Kwani katika siku ile nitakapompatiliza Israeli makosa yake, nitazipatiliza pia madhabahu za Betheli, na pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali, na kuanguka chini. Amosi 3:14

"For in the day that I visit the transgressions of Israel on him, I will also visit the altars of Bethel; And the horns of the altar will be cut off, And fall to the ground.

Nami nitaipiga nyumba ya wakati wa baridi pamoja na nyumba ya wakati wa hari; na hizo nyumba za pembe zitaangamia, nazo nyumba kubwa zitakuwa na mwisho, asema Bwana. Amosi 3:15

I will strike the winter house with the summer house; And the houses of ivory will perish, And the great houses will have an end," says Yahweh.