Amosi 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Amosi 6 (Swahili) Amos 6 (English)

Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria, watu mashuhuri wa taifa lililo la kwanza, ambao nyumba ya Israeli huwaendea. Amosi 6:1

Woe to those who are at ease in Zion, And to those who are secure on the mountain of Samaria, The notable men of the chief of the nations, To whom the house of Israel come!

Piteni hata Kalne, mkaone; tena tokea huko enendeni hata Hamathi iliyo kuu; kisha shukeni hata Gathi ya Wafilisti; je! Ninyi ni bora kuliko falme hizi? Au mpaka wao ni mkubwa kuliko mpaka wenu? Amosi 6:2

Go to Calneh, and see; And from there go to Hamath the great; Then go down to Gath of the Philistines. Are they better than these kingdoms? Or is their border greater than your border?

Ninyi mnaoiweka mbali siku hiyo mbaya, na kulileta karibu kao la udhalimu; Amosi 6:3

Those who put far away the evil day, And cause the seat of violence to come near;

ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe, na kujinyosha juu ya masemadari yenu; ninyi mnaokula wana-kondoo wa kundi, na ndama waliomo zizini; Amosi 6:4

Who lie on beds of ivory, And stretch themselves on their couches, And eat the lambs out of the flock, And the calves out of the midst of the stall;

ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi; Amosi 6:5

Who strum on the strings of a harp; Who invent for themselves instruments of music, like David;

ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu. Amosi 6:6

Who drink wine in bowls, And anoint themselves with the best oils; But they are not grieved for the affliction of Joseph.

Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani pamoja na wa kwanza watakaokwenda utumwani, na kelele za machezo za hao waliojinyosha zitakoma. Amosi 6:7

Therefore they will now go captive with the first who go captive; And the feasting and lounging will end.

Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema Bwana, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake. Amosi 6:8

"The Lord Yahweh has sworn by himself," says Yahweh, the God of hosts: "I abhor the pride of Jacob, And detest his fortresses. Therefore I will deliver up the city with all that is in it.

Hata itakuwa, wakisalia wanaume kumi katika nyumba moja, watakufa. Amosi 6:9

It will happen, if there remain ten men in one house, That they shall die.

Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu ye yote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la Bwana. Amosi 6:10

"When a man's relative carries him, even he who burns him, to bring bodies out of the house, and asks him who is in the innermost parts of the house, 'Is there yet any with you?' And he says, 'No;' then he will say, 'Hush! Indeed we must not mention the name of Yahweh.'

Kwa maana, angalia, Bwana atoa amri, na nyumba kubwa itapigwa na kuwa na mahali palipobomolewa, na nyumba ndogo nayo itapigwa iwe na nyufa. Amosi 6:11

"For, behold, Yahweh commands, and the great house will be smashed to pieces, And the little house into bits.

Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima na ng'ombe huko? Hata mmegeuza hukumu kuwa uchungu, na matunda ya haki kuwa pakanga; Amosi 6:12

Do horses run on the rocky crags? Does one plow there with oxen? But you have turned justice into poison, And the fruit of righteousness into bitterness;

ninyi mnaolifurahia jambo lisilo na maana, msemao, Je! Hatukujipatia pembe kwa nguvu zetu wenyewe? Amosi 6:13

You who rejoice in a thing of nothing, who say, 'Haven't we taken for ourselves horns by our own strength?'

Maana, angalia, nitaondokesha taifa juu yenu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana, Mungu wa majeshi, nao watawatesa ninyi toka mahali pa kuingilia katika Hamathi hata kijito cha Araba. Amosi 6:14

For, behold, I will raise up against you a nation, house of Israel," Says Yahweh, the God of hosts; "And they will afflict you from the entrance of Hamath to the brook of the Arabah."