1 Timotheo 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Timotheo 3 (Swahili) 1st Timothy 3 (English)

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. 1 Timotheo 3:1

This is a faithful saying: if a man seeks the office of an overseer{Or, bishop}, he desires a good work.

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; 1 Timotheo 3:2

The overseer therefore must be without reproach, the husband of one wife, temperate, sensible, modest, hospitable, good at teaching;

si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; 1 Timotheo 3:3

not a drinker, not violent, not greedy for money, but gentle, not quarrelsome, not covetous;

mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 1 Timotheo 3:4

one who rules his own house well, having children in subjection with all reverence;

(yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) 1 Timotheo 3:5

(but if a man doesn't know how to rule his own house, how will he take care of the assembly of God?)

Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 1 Timotheo 3:6

not a new convert, lest being puffed up he fall into the same condemnation as the devil.

Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. 1 Timotheo 3:7

Moreover he must have good testimony from those who are outside, to avoid falling into reproach and the snare of the devil.

Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu. 1 Timotheo 3:8

Deacons{The word for "deacons" literally means "servants."}, in the same way, must be reverent, not double-tongued, not addicted to much wine, not greedy for money;

wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. 1 Timotheo 3:9

holding the mystery of the faith in a pure conscience.

Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. 1 Timotheo 3:10

Let them also first be tested; then let them serve as deacons, if they are blameless.

Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. 1 Timotheo 3:11

Their wives in the same way must be reverent, not slanderers, temperate, faithful in all things.

Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. 1 Timotheo 3:12

Let deacons be husbands of one wife, ruling their children and their own houses well.

Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. 1 Timotheo 3:13

For those who have served well as deacons gain to themselves a good standing, and great boldness in the faith which is in Christ Jesus.

Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. 1 Timotheo 3:14

These things I write to you, hoping to come to you shortly;

Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 1 Timotheo 3:15

but if I wait long, that you may know how men ought to behave themselves in the house of God, which is the assembly of the living God, the pillar and ground of the truth.

Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu. 1 Timotheo 3:16

Without controversy, the mystery of godliness is great: God was revealed in the flesh, Justified in the spirit, Seen by angels, Preached among the nations, Believed on in the world, And received up in glory.