1 Timotheo 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Timotheo 2 (Swahili) 1st Timothy 2 (English)

Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 1 Timotheo 2:1

I exhort therefore, first of all, that petitions, prayers, intercessions, and givings of thanks, be made for all men:

kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 1 Timotheo 2:2

for kings and all who are in high places; that we may lead a tranquil and quiet life in all godliness and reverence.

Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 1 Timotheo 2:3

For this is good and acceptable in the sight of God our Savior;

ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. 1 Timotheo 2:4

who desires all people to be saved and come to full knowledge of the truth.

Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 1 Timotheo 2:5

For there is one God, and one mediator between God and men, the man Christ Jesus,

ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 1 Timotheo 2:6

who gave himself as a ransom for all; the testimony in its own times;

Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli. 1 Timotheo 2:7

to which I was appointed a preacher and an apostle (I am telling the truth in Christ, not lying), a teacher of the Gentiles in faith and truth.

Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 1 Timotheo 2:8

I desire therefore that the men in every place pray, lifting up holy hands without wrath and doubting.

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 1 Timotheo 2:9

In the same way, that women also adorn themselves in decent clothing, with modesty and propriety; not just with braided hair, gold, pearls, or expensive clothing;

bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 1 Timotheo 2:10

but (which becomes women professing godliness) with good works.

Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 1 Timotheo 2:11

Let a woman learn in quietness with all subjection.

Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 1 Timotheo 2:12

But I don't permit a woman to teach, nor to exercise authority over a man, but to be in quietness.

Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 1 Timotheo 2:13

For Adam was first formed, then Eve.

Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 1 Timotheo 2:14

Adam wasn't deceived, but the woman, being deceived, has fallen into disobedience;

Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

1 Timotheo 2:15

but she will be saved through her child-bearing, if they continue in faith, love, and sanctification with sobriety.