1 Timotheo 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Timotheo 1 (Swahili) 1st Timothy 1 (English)

Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu; 1 Timotheo 1:1

Paul, an apostle of Christ Jesus according to the commandment of God our Savior, and Christ Jesus our hope;

kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 1 Timotheo 1:2

to Timothy, my true child in faith: Grace, mercy, and peace, from God our Father and Christ Jesus our Lord.

Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine; 1 Timotheo 1:3

As I exhorted you to stay at Ephesus when I was going into Macedonia, that you might charge certain men not to teach a different doctrine,

wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo. 1 Timotheo 1:4

neither to pay attention to myths and endless genealogies, which cause disputes, rather than God's stewardship, which is in faith--

Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. 1 Timotheo 1:5

but the end of the charge is love, out of a pure heart and a good conscience and unfeigned faith;

Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili; 1 Timotheo 1:6

from which things some, having missed the mark, have turned aside to vain talking;

wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti. 1 Timotheo 1:7

desiring to be teachers of the law, though they understand neither what they say, nor about what they strongly affirm.

Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali; 1 Timotheo 1:8

But we know that the law is good, if a man uses it lawfully,

akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji, 1 Timotheo 1:9

as knowing this, that law is not made for a righteous man, but for the lawless and insubordinate, for the ungodly and sinners, for the unholy and profane, for murderers of fathers and murderers of mothers, for manslayers,

na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima; 1 Timotheo 1:10

for the sexually immoral, for homosexuals, for slave-traders, for liars, for perjurers, and for any other thing contrary to the sound doctrine;

kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana. 1 Timotheo 1:11

according to the Gospel of the glory of the blessed God, which was committed to my trust.

Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake; 1 Timotheo 1:12

And I thank him who enabled me, Christ Jesus our Lord, because he counted me faithful, appointing me to service;

ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. 1 Timotheo 1:13

although I was before a blasphemer, a persecutor, and insolent. However, I obtained mercy, because I did it ignorantly in unbelief.

Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu. 1 Timotheo 1:14

The grace of our Lord abounded exceedingly with faith and love which is in Christ Jesus.

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. 1 Timotheo 1:15

The saying is faithful and worthy of all acceptance, that Christ Jesus came into the world to save sinners; of whom I am chief.

Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele. 1 Timotheo 1:16

However, for this cause I obtained mercy, that in me first, Jesus Christ might display all his patience, for an example of those who were going to believe in him for eternal life.

Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina. 1 Timotheo 1:17

Now to the King eternal, immortal, invisible, to God who alone is wise, be honor and glory forever and ever. Amen.

Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri; 1 Timotheo 1:18

This charge I commit to you, my child Timothy, according to the prophecies which led the way to you, that by them you may wage the good warfare;

uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani. 1 Timotheo 1:19

holding faith and a good conscience; which some having thrust away made a shipwreck concerning the faith;

Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu. 1 Timotheo 1:20

of whom is Hymenaeus and Alexander; whom I delivered to Satan, that they might be taught not to blaspheme.