Sifa Lyrics

Wewe ni Mkuu by Sounds Of Afrika Music cover art

Sounds Of Afrika Music - Wewe ni Mkuu Lyrics

Artist:
Sounds Of Afrika Music

Lyrics

Umevikwa Utukufu
Na heshima ni zako
Enzi yako, na mamlaka
Zinadumu milele


Nitakiri, kwa kinywa changu
Kwamba wewe ni Mungu mkuu
Viumbe vyote, Vikushukuru
Vikisema wewe ni Mkuu


Hakika, wewe ni Mungu
Umetenda, maajabu 
Umejaa, hekima na rehema
Hakika wewe ni mkuu


Khalvari, kasulubiwa, ili mimi niishi
Dhambi zangu, kazisafisha
Sasa mimi ni huru
Kwako wewe, nitasimama


Mwamba imara asiyeshindwa 
Mwili wangu, na nafsi yangu
Maisha yangu, natoa kwako 


Video