Sifa Lyrics

Raha by Neema Mwaipopo cover art

Neema Mwaipopo - Raha Lyrics

Artist:
Neema Mwaipopo

Lyrics

Adui zangu, nimewasamehe bure
Na moyoni mwangu sina kinyongo tena
Watesi wangu nimewasamehe bure
Na moyoni mwangu, nimejaza msamaha


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Matukio ni mengi katika dunia
Na wanaotuudhi ni wengi mno
Na wengine ni wale wa karibu nasi
Tutaweka wangapi katika mioyo


Matukio ni mengi katika dunia
Na wanaotuudhi ni wengi mno
Na wengine ni wale wa karibu nasi
Tutaweka wangapi katika mioyo


Mwisho mioyo yetu ipasuke bure
Mwisho sura zetu, zizeeke mapema


Mwisho mioyo yetu ipasuke bure
Mwisho sura zetu, zizeeke mapema
Rahaaaa jipe mwenyewe...


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Ugomvi ni mbaya, huumiza moyo
Kinyongo ni hatari, hukosesha raha
Kwa nini ujitese kwa mambo yapitayo
Hao ni wanadamu, wanapita tu


Ugomvi ni mbaya, huumiza moyo
Kinyongo ni hatari, hukosesha raha
Kwa nini ujitese kwa mambo yapitayo
Hao ni wanadamu, wanapita tu


Hata wasipotubu, wewe wasamehe
Usijinyime raha jipe mwenyewe


Hata wasipotubu, wewe wasamehe
Usijinyime raha, jipe mwenyewe
Nasema raha jipe mwenyewe...


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Adui zako, wewe wasamehe bure
Na moyoni mwako usiwe na kinyongo
Watesi wako we wasamehe bure
Na moyoni mwako ujaze msamaha


Binadamu wengine ni wakorofi
Hata ukinyamaza, watasema tu
Ajira yao kubwa ni masengenyo
Usigombane nao, utakosa nguvu


Binadamu wengine ni wakorofi
Hata ukinyamaza, watasema tu
Ajira yao kubwa ni masengenyo
Usigombane nao, utakosa nguvu


Ukifanikiwa wanakasirika
Kama waliyachangia, mafanikio yako
Mungu akikuinua mioyo inawauma
Kama walijuwa agano lako na Mungu
Ukifanikiwa wanakasirika
Kama waliyachangia, mafanikio yako
Mungu akikuinua mioyo inawauma inawakera
Kama walijuwa agano lako na Mungu
Mie Raha Najipa Mwenyewe...


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Usikubali moyo upasuke bure
Usikubali sura izeeke mapema
Usikubali moyo upasuke bure
Kisha sura izeeke mapema
Wewe raha jipe mwenyewe


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Moyo wangu una amani
Moyo wangu hauna mashaka
Moyo wangu una furaha
Moyo wangu hauna kinyongo


Video