Mwenyehaki - Roho Yangu Lyrics
Contents:
Bwana Mungu nashangaa kabisa
Nikifikiri jinsi ulivyo
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia
Viumbavyo kwa uwezo wako
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Nikitembea pote duniani
Ndege huimba nawasikia
Milima hupendeza macho sana
Upepo nao nafurahia
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Nikikumbuka vile wewe Mungu
Ulivyompeleka mwanao
Afe azichukue dhambi zetu
Kuyatambua ni vigumu mno
Yesu Mwokozi atakaporudi
Kunichukua kwenda mbinguni
Nitaimba sifa zako milele
Wote wajue jinsi ulivyo
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu