Sifa Lyrics

Bariki Kenya by Kamnjoro cover art

Kamnjoro - Bariki Kenya Lyrics

Artist:
Kamnjoro

Lyrics

Mwenyezi Mungu napiga magoti
Nikiombea nchi yangu kenya
Amani upendo na umoja, Kenya yetu amani tele
ufisadi ubinafsi ukabila, adui zetu Kenya wanatutesa
vijana wetu umewamalika, kweli shetani kaamulia Kenya

Ni wengi wametuacha, wengi wamelala salama
wengi wanateseka, ee Mungu ilinde Kenya

Baba kuwa unatupenda, unatujali tena unatuwaza
Hawa wachafu wanachafua Kenya
Tumalizie daddy safisha Kenya
Shetani hauna uwezo, kazi yako kuchanganya watu
kuharibu na kumaliza, nakuamuru sasa uhame Kenya

Ni wengi wametuacha, wengi wamelala salama
wengi wanateseka, ee Mungu ilinde Kenya

Na tena narudisha shukrani kwa viongozi Baba uliotupa
Kwa kuwa mi tena ni wakuheshimu, Bariki kenya baba tufurahie
Roho wa Mungu, Bariki kenya
Daima kenya, amani tele
Kupingana hatuna, sote ni wakenya
Mliolala, laleni salama
Mwenyezi Mungu, Bariki Kenya

Ni wengi wametuacha, wengi wamelala salama
wengi wanateseka, ee Mungu ilinde Kenya
Na tena narudisha shukrani kwa viongozi Baba uliotupa
Kwa kuwa mi tena ni wakuheshimu, Bariki kenya baba tufurahie
Roho wa Mungu, Bariki kenya
amani tele, sote ni wakenya, laleni salama
Mwenyezi Mungu, Bariki Kenya

Video