.Nyimbo na tuziimbe tena za alivyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele.
Twonane milele, Twonane bandarini kule;
Twonane milele, Twonane bandarini kule.
Hupozwa kila aoshwaye, Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye Vya Yesu mbinguni milele.
Twonane milele, Twonane bandarini kule;
Twonane milele, Twonane bandarini kule.
Hata sasa hufurahia Tamu yake mapenzi yale,
Je,kwake tukifikilia, Kutofarakana milele?
Twonane milele, Twonane bandarini kule;
Twonane milele, Twonane bandarini kule.
Twende mbele kwa jina lake, Hata aje mwokozi yule,
Atatukaribisha kwake, Tutawale naye milele.
Twonane milele, Twonane bandarini kule;
Twonane milele, Twonane bandarini kule.
Sauti zetu tuinue Kumsifu Mwokozi yule,
Ili watu wote wajue Wokovu u kwake milele.
Twonane milele, Twonane bandarini kule;
Twonane milele, Twonane bandarini kule.
Write a review of Twonane Milele - Nyimbo Na Tuziimbe Tena :
dinu zeno tuonane milele 1 week ago
Then we who are still living will be taken up together with them into the clouds to see the Lord in the air: and so will we be for ever with the Lord.