Wimbo Ulio Bora 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wimbo Ulio Bora 3 (Swahili) Song Of Songs 3 (English)

Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate. Wimbo Ulio Bora 3:1

By night on my bed, I sought him whom my soul loves. I sought him, but I didn't find him.

Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Wimbo Ulio Bora 3:2

I will get up now, and go about the city; In the streets and in the squares I will seek him whom my soul loves. I sought him, but I didn't find him.

Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? Wimbo Ulio Bora 3:3

The watchmen who go about the city found me; "Have you seen him whom my soul loves?"

Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. Wimbo Ulio Bora 3:4

I had scarcely passed from them, When I found him whom my soul loves. I held him, and would not let him go, Until I had brought him into my mother's house, Into the chamber of her who conceived me.

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. Wimbo Ulio Bora 3:5

I adjure you, daughters of Jerusalem, By the roes, or by the hinds of the field, That you not stir up, nor awaken love, Until it so desires.

Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi? Wimbo Ulio Bora 3:6

Who is this who comes up from the wilderness like pillars of smoke, Perfumed with myrrh and frankincense, With all spices of the merchant?

Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli. Wimbo Ulio Bora 3:7

Behold, it is Solomon's carriage! Sixty mighty men are around it, Of the mighty men of Israel.

Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku. Wimbo Ulio Bora 3:8

They all handle the sword, and are expert in war. Every man has his sword on his thigh, Because of fear in the night.

Mfalme Sulemani alijifanyizia machela Ya miti ya Lebanoni; Wimbo Ulio Bora 3:9

King Solomon made himself a carriage Of the wood of Lebanon.

Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu. Wimbo Ulio Bora 3:10

He made its pillars of silver, Its bottom of gold, its seat of purple, Its midst being paved with love, From the daughters of Jerusalem.

Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alivyovikwa na mamaye, Siku ya maposo yake, Siku ya furaha ya moyo wake. Wimbo Ulio Bora 3:11

Go forth, you daughters of Zion, and see king Solomon, With the crown with which his mother has crowned him, In the day of his weddings, In the day of the gladness of his heart. Lover