Zekaria 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zekaria 5 (Swahili) Zechariah 5 (English)

Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo. Zekaria 5:1

Then again I lifted up my eyes, and saw, and, behold, a flying scroll.

Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi. Zekaria 5:2

He said to me, "What do you see?" I answered, "I see a flying scroll; its length is twenty cubits, and its breadth ten cubits."

Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili. Zekaria 5:3

Then he said to me, "This is the curse that goes out over the surface of the whole land; for everyone who steals shall be cut off according to it on the one side; and everyone who swears falsely shall be cut off according to it on the other side.

Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake. Zekaria 5:4

I will cause it to go out," says Yahweh of Hosts, "and it will enter into the house of the thief, and into the house of him who swears falsely by my name; and it will remain in the midst of his house, and will destroy it with its timber and its stones."

Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho. Zekaria 5:5

Then the angel who talked with me came forward, and said to me, "Lift up now your eyes, and see what is this that is appearing."

Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote; Zekaria 5:6

I said, "What is it?" He said, "This is the ephah{ An ephah is a measure of volume of about 22 litres, 5.8 U. S. gallons, 4.8 imperial gallons, or a bit more than half a bushel. } basket that is appearing." He said moreover, "This is their appearance in all the land

na tazama, talanta ya risasi iliinuliwa; na tazama, mwanamke akaaye katikati ya hiyo efa. Zekaria 5:7

(and, behold, a talent{A talent is a weight of about 34 kilograms or 75 pounds.} of lead was lifted up); and this is a woman sitting in the midst of the ephah basket."

Akasema, Huyu ni Uovu; akamtupa chini katikati ya ile efa; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa. Zekaria 5:8

He said, "This is Wickedness;" and he threw her down into the midst of the ephah basket; and he threw the weight of lead on its mouth.

Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu. Zekaria 5:9

Then lifted I up my eyes, and saw, and, behold, there were two women, and the wind was in their wings. Now they had wings like the wings of a stork, and they lifted up the ephah basket between earth and the sky.

Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? Zekaria 5:10

Then said I to the angel who talked with me, "Where are these carrying the ephah basket?"

Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari; tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe. Zekaria 5:11

He said to me, "To build her a house in the land of Shinar. When it is prepared, she will be set there in her own place."