Nehemia 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 8 (Swahili) Nehemiah 8 (English)

Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha torati ya Musa, Bwana aliyowaamuru Israeli. Nehemia 8:1

All the people gathered themselves together as one man into the broad place that was before the water gate; and they spoke to Ezra the scribe to bring the book of the law of Moses, which Yahweh had commanded to Israel.

Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba. Nehemia 8:2

Ezra the priest brought the law before the assembly, both men and women, and all who could hear with understanding, on the first day of the seventh month.

Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha torati. Nehemia 8:3

He read therein before the broad place that was before the water gate from early morning until midday, in the presence of the men and the women, and of those who could understand; and the ears of all the people were [attentive] to the book of the law.

Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu. Nehemia 8:4

Ezra the scribe stood on a pulpit of wood, which they had made for the purpose; and beside him stood Mattithiah, and Shema, and Anaiah, and Uriah, and Hilkiah, and Maaseiah, on his right hand; and on his left hand, Pedaiah, and Mishael, and Malchijah, and Hashum, and Hashbaddanah, Zechariah, [and] Meshullam.

Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama; Nehemia 8:5

Ezra opened the book in the sight of all the people; (for he was above all the people;) and when he opened it, all the people stood up:

Ezra akamhimidi Bwana, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu Bwana kifudifudi. Nehemia 8:6

and Ezra blessed Yahweh, the great God. All the people answered, Amen, Amen, with the lifting up of their hands: and they bowed their heads, and worshiped Yahweh with their faces to the ground.

Tena Yeshua, na Bani, na Sherebia, na Yamini, na Akubu, na Shabethai, na Hodai, na Maaseya, na Kelita, na Azaria, na Yozabadi, na Hanani, na Pelaya, nao ni Walawi, wakawafahamisha watu torati; na watu wakasimama mahali pao. Nehemia 8:7

Also Jeshua, and Bani, and Sherebiah, Jamin, Akkub, Shabbethai, Hodiah, Maaseiah, Kelita, Azariah, Jozabad, Hanan, Pelaiah, and the Levites, caused the people to understand the law: and the people [stood] in their place.

Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa. Nehemia 8:8

They read in the book, in the law of God, distinctly; and they gave the sense, so that they understood the reading.

Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati. Nehemia 8:9

Nehemiah, who was the governor, and Ezra the priest the scribe, and the Levites who taught the people, said to all the people, This day is holy to Yahweh your God; don't mourn, nor weep. For all the people wept, when they heard the words of the law.

Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. Nehemia 8:10

Then he said to them, Go your way, eat the fat, and drink the sweet, and send portions to him for whom nothing is prepared; for this day is holy to our Lord: neither be you grieved; for the joy of Yahweh is your strength.

Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike. Nehemia 8:11

So the Levites stilled all the people, saying, Hold your peace, for the day is holy; neither be you grieved.

Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa. Nehemia 8:12

All the people went their way to eat, and to drink, and to send portions, and to make great mirth, because they had understood the words that were declared to them.

Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababa za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kuyasikiliza maneno ya torati. Nehemia 8:13

On the second day were gathered together the heads of fathers' [houses] of all the people, the priests, and the Levites, to Ezra the scribe, even to give attention to the words of the law.

Wakaona ya kuwa imeandikwa katika torati, jinsi Bwana alivyoamuru kwa mkono wa Musa, ya kwamba wana wa Israeli wakae katika vibanda, katika sikukuu ya mwezi wa saba; Nehemia 8:14

They found written in the law, how that Yahweh had commanded by Moses, that the children of Israel should dwell in booths in the feast of the seventh month;

na ya kwamba wahubiri na kutangaza katika miji yao yote, na katika Yerusalemu, kusema, Enendeni mlimani, mkalete matawi ya mzeituni, na matawi ya mzeituni-mwitu, na matawi ya mihadasi, na matawi ya mitende, na matawi ya miti minene, ili kufanya vibanda, kama ilivyoandikwa. Nehemia 8:15

and that they should publish and proclaim in all their cities, and in Jerusalem, saying, Go forth to the mountain, and get olive branches, and branches of wild olive, and myrtle branches, and palm branches, and branches of thick trees, to make booths, as it is written.

Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajifanyizia vibanda, kila mtu juu ya dari ya nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu. Nehemia 8:16

So the people went forth, and brought them, and made themselves booths, everyone on the roof of his house, and in their courts, and in the courts of the house of God, and in the broad place of the water gate, and in the broad place of the gate of Ephraim.

Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakafanyiza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tokea siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hata siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana. Nehemia 8:17

All the assembly of those who were come again out of the captivity made booths, and lived in the booths; for since the days of Jeshua the son of Nun to that day the children of Israel had not done so. There was very great gladness.

Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hata siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa. Nehemia 8:18

Also day by day, from the first day to the last day, he read in the book of the law of God. They kept the feast seven days; and on the eighth day was a solemn assembly, according to the ordinance.