Malaki 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Malaki 1 (Swahili) Malachi 1 (English)

Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki Malaki 1:1

An oracle: the word of Yahweh to Israel by Malachi.

Nimewapenda ninyi, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema Bwana; ila nimempenda Yakobo; Malaki 1:2

"I have loved you," says Yahweh. Yet you say, "How have you loved us?" "Wasn't Esau Jacob's brother?" says Yahweh, "Yet I loved Jacob;

bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani. Malaki 1:3

but Esau I hated, and made his mountains a desolation, and gave his heritage to the jackals of the wilderness."

Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; Bwana wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao Bwana anawaghadhabikia milele. Malaki 1:4

Whereas Edom says, "We are beaten down, but we will return and build the waste places;" thus says Yahweh of Hosts, "They shall build, but I will throw down; and men will call them 'The Wicked Land,' even the people against whom Yahweh shows wrath forever."

Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, Bwana ndiye mkuu kupita mpaka wa Israeli. Malaki 1:5

Your eyes will see, and you will say, "Yahweh is great--even beyond the border of Israel!"

Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Malaki 1:6

"A son honors his father, and a servant his master. If I am a father, then where is my honor? And if I am a master, where is the respect due me? Says Yahweh of Hosts to you, priests, who despise my name. You say, 'How have we despised your name?'

Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya Bwana ni kitu cha kudharauliwa. Malaki 1:7

You offer polluted bread on my altar. You say, 'How have we polluted you?' In that you say, 'Yahweh's table contemptible.'

Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema Bwana wa majeshi. Malaki 1:8

When you offer the blind for sacrifice, isn't that evil? And when you offer the lame and sick, isn't that evil? Present it now to your governor! Will he be pleased with you? Or will he accept your person?" says Yahweh of Hosts.

Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema Bwana wa majeshi. Malaki 1:9

"Now, please entreat the favor of God, that he may be gracious to us. With this, will he accept any of you?" says Yahweh of Hosts.

Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema Bwana wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu. Malaki 1:10

"Oh that there were one among you who would shut the doors, that you might not kindle fire on my altar in vain! I have no pleasure in you," says Yahweh of hosts, "neither will I accept an offering at your hand.

Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika Mataifa, asema Bwana wa majeshi. Malaki 1:11

For from the rising of the sun even to the going down of the same, my name is great among the nations, and in every place incense will be offered to my name, and a pure offering: for my name is great among the nations," says Yahweh of Hosts.

Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya Bwana imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. Malaki 1:12

"But you profane it, in that you say, 'Yahweh's table is polluted, and its fruit, even its food, is contemptible.'

Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema Bwana wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana. Malaki 1:13

You say also, 'Behold, what a weariness it is!' and you have sniffed at it," says Yahweh of Hosts; "and you have brought that which was taken by violence, the lame, and the sick; thus you bring the offering. Should I accept this at your hand?" says Yahweh.

Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema Bwana wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa. Malaki 1:14

"But the deceiver is cursed, who has in his flock a male, and vows, and sacrifices to the Lord a blemished thing; for I am a great King," says Yahweh of hosts, "and my name is awesome among the nations."