Yona 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yona 3 (Swahili) Jonah 3 (English)

Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, Yona 3:1

The word of Yahweh came to Jonah the second time, saying,

Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Yona 3:2

"Arise, go to Nineveh, that great city, and preach to it the message that I give you."

Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona 3:3

So Jonah arose, and went to Nineveh, according to the word of Yahweh. Now Nineveh was an exceedingly great city, three days' journey across.

Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Yona 3:4

Jonah began to enter into the city a day's journey, and he cried out, and said, "Yet forty days, and Nineveh shall be overthrown!"

Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Yona 3:5

The people of Nineveh believed God; and they proclaimed a fast, and put on sackcloth, from the greatest of them even to the least of them.

Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Yona 3:6

The news reached the king of Nineveh, and he arose from his throne, and took off his royal robe, covered himself with sackcloth, and sat in ashes.

Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; Yona 3:7

He made a proclamation and published through Nineveh by the decree of the king and his nobles, saying, "Let neither man nor animal, herd nor flock, taste anything; let them not feed, nor drink water;

bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Yona 3:8

but let them be covered with sackcloth, both man and animal, and let them cry mightily to God. Yes, let them turn everyone from his evil way, and from the violence that is in his hands.

Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? Yona 3:9

Who knows whether God will not turn and repent, and turn away from his fierce anger, so that we might not perish?"

Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende. Yona 3:10

God saw their works, that they turned from their evil way. God repented of the evil which he said he would do to them, and he didn't do it.