Hagai 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hagai 2 (Swahili) Haggai 2 (English)

Katika mwezi wa saba, siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema, Hagai 2:1

In the seventh month, in the twenty-first day of the month, the Word of Yahweh came by Haggai the prophet, saying,

Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hayo mabaki ya watu, ukisema, Hagai 2:2

"Speak now to Zerubbabel, the son of Shealtiel, governor of Judah, and to Joshua, the son of Jehozadak, the high priest, and to the remnant of the people, saying,

Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu? Hagai 2:3

'Who is left among you who saw this house in its former glory? How do you see it now? Isn't it in your eyes as nothing?

Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi; Hagai 2:4

Yet now be strong, Zerubbabel,' says Yahweh. 'Be strong, Joshua, son of Jehozadak, the high priest. Be strong, all you people of the land,' says Yahweh, 'and work, for I am with you,' says Yahweh of Hosts.

kama neno lile nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope. Hagai 2:5

This is the word that I covenanted with you when you came out of Egypt, and my Spirit lived among you. Don't be afraid.'

Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; Hagai 2:6

For this is what Yahweh of Hosts says: 'Yet once, it is a little while, and I will shake the heavens, the earth, the sea, and the dry land;

nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. Hagai 2:7

and I will shake all nations. The precious things of all nations will come, and I will fill this house with glory, says Yahweh of Hosts.

Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi. Hagai 2:8

The silver is mine, and the gold is mine,' says Yahweh of Hosts.

Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi. Hagai 2:9

'The latter glory of this house will be greater than the former,' says Yahweh of Hosts; 'and in this place will I give peace,' says Yahweh of Hosts."

Siku ya ishirini na nne, ya mwezi wa kenda, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema, Hagai 2:10

In the twenty-fourth day of the ninth month, in the second year of Darius, the Word of Yahweh came by Haggai the prophet, saying,

Bwana wa majeshi asema hivi, Waulizeni sasa makuhani katika habari ya sheria, mkisema, Hagai 2:11

"Thus says Yahweh of Hosts: Ask now the priests concerning the law, saying,

Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye akagusa kwa upindo wake mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula cho chote, je! Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La. Hagai 2:12

'If someone carries holy meat in the fold of his garment, and with his fold touches bread, stew, wine, oil, or any food, will it become holy?'" The priests answered, "No."

Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je! Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi. Hagai 2:13

Then Haggai said, "If one who is unclean by reason of a dead body touch any of these, will it be unclean?" The priests answered, "It will be unclean."

Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema Bwana; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi. Hagai 2:14

Then Haggai answered, "'So is this people, and so is this nation before me,' says Yahweh; 'and so is every work of their hands. That which they offer there is unclean.

Na sasa nawaomba, tafakarini; tangu siku hii na siku zilizopita; kabla halijatiwa bado jiwe juu ya jiwe katika nyumba ya Bwana; Hagai 2:15

Now, please consider from this day and backward, before a stone was laid on a stone in the temple of Yahweh.

katika wakati huo wote, mtu alipofikia chungu ya vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia shinikizo apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu. Hagai 2:16

Through all that time, when one came to a heap of twenty measures, there were only ten. When one came to the wine vat to draw out fifty, there were only twenty.

Naliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunielekea mimi, asema Bwana. Hagai 2:17

I struck you with blight, mildew, and hail in all the work of your hands; yet you didn't turn to me,' says Yahweh.

Tafakarini, nawaomba; tangu siku hii ya leo na siku zijazo; tangu siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kenda, naam, tangu siku hiyo ulipowekwa msingi wa hekalu la Bwana tafakarini haya. Hagai 2:18

'Consider, please, from this day and backward, from the twenty-fourth day of the ninth month, since the day that the foundation of Yahweh's temple was laid, consider it.

Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki. Hagai 2:19

Is the seed yet in the barn? Yes, the vine, the fig tree, the pomegranate, and the olive tree haven't brought forth. From this day will I bless you.'"

Kisha neno la Bwana likamjia Hagai mara ya pili, siku ya ishirini na nne ya mwezi, kusema, Hagai 2:20

The Word of Yahweh came the second time to Haggai in the twenty-fourth day of the month, saying,

Sema na Zerubabeli, liwali wa Yuda, ukisema, Nitazitikisa mbingu na dunia; Hagai 2:21

"Speak to Zerubbabel, governor of Judah, saying, 'I will shake the heavens and the earth.

nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake. Hagai 2:22

I will overthrow the throne of kingdoms. I will destroy the strength of the kingdoms of the nations. I will overthrow the chariots, and those who ride in them. The horses and their riders will come down, everyone by the sword of his brother.

Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema Bwana, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi. Hagai 2:23

In that day, says Yahweh of Hosts, will I take you, Zerubbabel, my servant, the son of Shealtiel,' says Yahweh, 'and will make you as a signet, for I have chosen you,' says Yahweh of Hosts."