Hagai 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hagai 1 (Swahili) Haggai 1 (English)

Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema, Hagai 1:1

In the second year of Darius the king, in the sixth month, in the first day of the month, the Word of Yahweh came by Haggai, the prophet, to Zerubbabel, the son of Shealtiel, governor of Judah, and to Joshua, the son of Jehozadak, the high priest, saying,

Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana. Hagai 1:2

"This is what Yahweh of Hosts says: These people say, 'The time hasn't yet come, the time for Yahweh's house to be built.'"

Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Hagai 1:3

Then the Word of Yahweh came by Haggai, the prophet, saying,

Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika? Hagai 1:4

"Is it a time for you yourselves to dwell in your paneled houses, while this house lies waste?

Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Hagai 1:5

Now therefore this is what Yahweh of Hosts says: Consider your ways.

Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. Hagai 1:6

You have sown much, and bring in little. You eat, but you don't have enough. You drink, but you aren't filled with drink. You clothe yourselves, but no one is warm, and he who earns wages earns wages to put them into a bag with holes in it."

Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Hagai 1:7

This is what Yahweh of Hosts says: "Consider your ways.

Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana. Hagai 1:8

Go up to the mountain, bring wood, and build the house. I will take pleasure in it, and I will be glorified," says Yahweh.

Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. Hagai 1:9

"You looked for much, and, behold, it came to little; and when you brought it home, I blew it away. Why?" says Yahweh of Hosts, "Because of my house that lies waste, while each of you is busy with his own house.

Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake. Hagai 1:10

Therefore for your sake the heavens withhold the dew, and the earth withholds its fruit.

Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono. Hagai 1:11

I called for a drought on the land, on the mountains, on the grain, on the new wine, on the oil, on that which the ground brings forth, on men, on cattle, and on all the labor of the hands."

Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana. Hagai 1:12

Then Zerubbabel, the son of Shealtiel, and Joshua, the son of Jehozadak, the high priest, with all the remnant of the people, obeyed the voice of Yahweh, their God, and the words of Haggai, the prophet, as Yahweh, their God, had sent him; and the people feared Yahweh.

Ndipo Hagai mjumbe wa Bwana, katika ujumbe wa Bwana, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema Bwana. Hagai 1:13

Then Haggai, Yahweh's messenger, spoke in Yahweh's message to the people, saying, "I am with you," says Yahweh.

Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao; Hagai 1:14

Yahweh stirred up the spirit of Zerubbabel, the son of Shealtiel, governor of Judah, and the spirit of Joshua, the son of Jehozadak, the high priest, and the spirit of all the remnant of the people; and they came and worked on the house of Yahweh of Hosts, their God,

katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa Dario mfalme. Hagai 1:15

in the twenty-fourth day of the month, in the sixth month, in the second year of Darius the king.